Ticker

6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) AFRIKA ATEMBELEA OFISI ZA TUCTA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa bara la Afrika Bi.Fanfan Kayirangwa amelipongeza Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kwa utendaji kazi wake hasa  upande wa kupigania haki za wafanyakazi wanapotekeleza majukumu yao.

Pongezi  hizo amezitoa leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi za TUCTA Jijini Dar es Salaam ambapo wamemuonesha Shughuli zao wanazozifanya na ameridhishwa na kazi wanazozifanya.

Aidha amesema kuwa ofisi yake itatoa ushirikiano katika kuwajengea uwezo wafanyakazi katika shirikisho hilo na kusaidia kuweka sawa mambo mbalimbali yanayohusu wafanyakazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Wa Shirika la kazi Dunia ILO ukanda wa Afrika Mashariki Bi Caroline Mogall amesema kutokana na mwangaza unaooneshwa na Tanzania kutokana na kauli mbalimbali za kiongozi Mkuu wa Nchi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ILO inatoa kipaumbele kikubwa kwa Tanzania kwani imeonyesha kuheshimu matakwa ya jamii(social justice).

Nae Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw.Mkunda amesema kuwa  wamemueleza kuhusu ajira za watoto ambapo lengo lao ni kukomesha ajira hizo kwa Kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali.

"Nchi yetu inashida kidogo kwa mfano migodini,kwenye mashamba Kuna mambo mbalimbali yanahusiana na ajira za watoto kwa jinsi gani tunaweza kuwa na programu mbalimbali ambazo zitaweza kusaidia kutoa Elimu na kuondokana na jambo hilo.Bw.Mkunda amesema.

Pamoja na hayo Bw.Mkunda ameeleza kuwa wamemwambia Mkurugenzi huyo kuhusiana na kukosa haki kwa wanawake katika maeneo ya kazi ambapo inapelekea wakati mwingine kuondolewa kazini ili serikali ibadirishe mfumo wake wa kisheria kwa lengo la kuwapatia haki

"Mfano unakuta mzazi anajifungua mtoto njiti muda anaopewa wa likizo unakuwa mfupi,ambapo inapelekea muda ukiisha mama anashindwa kumuhudumia mtoto wake nakufukuzwa kazi anaposhindwa kuhudhuria kazini.Bw.Mkunda ameeleza.

Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw.Hery Mkunda mara baada ya kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa Ukanda wa Afrika Mashariki Bi.Caroline Mugalla akizungumza mara baada Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw.Hery Mkunda akizungumza mara baada Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw.Hery Mkunda akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa Ukanda wa Afrika Mashariki Bi.Caroline Mugalla mara baada ya Mhe.Fanfan kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw.Hery Mkunda akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa Ukanda wa Afrika Mashariki Bi.Caroline Mugalla mara baada ya Mhe.Fanfan kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw.Hery Mkunda, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) upande wa Afrika, Mhe. Fanfan Kayirangwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa Ukanda wa Afrika Mashariki Bi.Caroline Mugalla wakiwa kwenye picha ya pamoja  na watumishi wa TUCTA mara baada ya Mhe.Fanfan kutembelea katika Ofisi za TUCTA leo Februari 6,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments