NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni amesema kuwa katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2023 matukio ya ajali na uhalifu yalikuwa machache tofauti na ilivyozoeleka, hii ni kutokana na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi kutoa ushirikiano katika kukabiliana na matukio hayo.
Ameyasema hayo leo Januari 4,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu usalama na vyombo vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
"Kwa kipindi cha mwaka 2023 hali ya usalama ilikuwa imeimarika na bado serikali inaendelea kuhakikisha usalama unaendelea kushamiri katika maeneo yote nchini". Amesema Waziri Masauni.
Aidha Waziri Masauni amesema kuwa Jeshi la Polisi limechukuwa hatua kwa matukio yote ya kiuhalifu ambayo yametokea hivi karibuni nchini, hivyo amewasihi wananchi kuwa na imani na jeshi lao na pia waweze kutoa ushirikiano pindi wanapoona ishara yoyote ya uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillius Wambura amesema kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kukabiliana na vijana wahalifu maarufu kwa jina la Panya Road kulingana na nguvu watakayotumia na hawapo tayari kushuhudia askari wanakufa wakiwa wanapambana na vijana hao.
Amesema kuwa polisi hulazimika kufa kwa sababu za msingi pindi anapokuwa anatetea haki za raia, hivyo nguvu anayoitumia kumdhibiti mhalifu hutegemeana na nguvu ya mhalifu.
"Askari hawapaswi kufanya uzembe wa aina yoyote wanapopambana na vijana hao na wanapaswa kutumia nguvu ya kadri katika kuwashughulikia na kuwadhibiti". Amesema IGP Wambura.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 4,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mambo mbalimbali yanayohusu usalama na vyombo vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 4,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mambo mbalimbali yanayohusu usalama na vyombo vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillius Wambura akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 4,2024 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments