Mhandisi Mwandamizi wa Umeme EWURA Kanda ya Kati, Nicholaus Kayombo (kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa VETA Singida namna ya kufanya maombi ya leseni kwa mfumo wa LOIS wakati wa mafunzo yaliyotolewa na EWURA chuoni hapo, leo 29 Jan 2024.
Wanafunzi wakifuatilia kwa umakini mafunzo kutoka kwa Wataalam wa EWURA juu ya udhibiti wa sekta ya umeme hususani masuala ya leseni leo, 29 .01. 24 katika chuo cha VETA Singida.
Na.Mwandishi Wetu-SINGIDA
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Singida kimeishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wake 100 wa fani ya Mifumo ya umeme.
Msajili wa Chuo hicho, Bw. Gelshom Maloda ameiomba EWURA kuendesha mafunzo ya mara kwa ili kuwajengea uwezo wanafunzi katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya sekta ya umeme.
Mhandisi mwandamizi Wa Umeme EWURA Kanda ya Kati, Nicholaus Kayombo, amewasilisha mada kuhusu masuala ya msingi ya Mifumo ya Umeme na Madaraja ya leseni za EWURA na namna ya kuomba leseni hizo kwa mtandao kupitia mfumo wa LOIS . Mfumo huo unapatikana katika tovuti ya Mamlaka www.ewura.go.tz.
Wanafunzi wamesisitiziwa umuhimu wa kumiliki leseni zinazotolewa na EWURA, ikiwa ni pamoja na utambulisho wa utalaamu wao, ubora wa huduma na usalama wa mali, watu na mazingira.
Mafunzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 29/1/2024, yameratibiwa na EWURA Kanda ya Kati, inayohudumia mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa na Morogoro.
0 Comments