Ticker

6/recent/ticker-posts

TGNP YAPENDEKEZA JESHI LA POLISI KUTOJIHUSISHA NA UCHAGUZI

    


Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi

Na Deogratius Temba, Dodoma

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umependekeza jeshi la Polisi Tanzania kutojihusisha na shughuli za kusimamia masuala ya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi badala yake kuundwe kikosi maalum cha cha uchaguzi chini ya Tume ya taifa ya Uchaguzi kitakachohudumu wakati wa mchakato wa uchaguzi pekee.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha maoni na mapendekezo ya maboresho ya miswaa mitatu (3), ambayo ni Mswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa mwaka 2023, Mswada wa sheria ya Uchaguzi wa Madiwani, wabunge na Rais wa mwaka 2023 na mswada wa marekebisho ya sheria ya mambo ya Vyama vya siasa ya mwaka 2019, ambao umewasilishwa Bungeni Oktoba 10,2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwama, ni vizuri Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC), ikaunda kikosi maalum cha kusimamia masuala ya usalama na ulinzi wakati wa uchaguzi, ambapo wahusika watajengewa uwezo namna ya kulinda usalama wa raia wote bila kusababisha changamto za uvunjivu wa Amani.

“.. Masuala ya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi ni lazima yajitokeze bayana katika sheria hii ili kudhibiti vitendo vya uvunjivu wa Amani, Tunapendekeza kifungu kipya cha 69 (1) kutakuwa na kikosi maalum cha Polisi watakaofanya kazi ya kulinda Amani na Utulivu wakati wote wa uchaguzi, kifungu cha 169 (2) Tume iwapatie mafunzo polisi wote wa kikosi cha Uchaguzi kuhusu masuala ya mchakato wa uchaguzi ikiwepo unyanyasanji na udhalilishaji wa kijinsia”, alisema Lilian

Pia, TGNP imependekeza kwamba, kuwepo kwa kifungu kipya cha 169 (3) kitakachosomeka kwamba, Polisi wa kikosi cha uchaguzi watakula kiapo cha uaminifu, na uadilifu mbele ya Hakimu wa mahakama ya mwanzo kabla ya kuanza majukumu ya kulinda usalama kwenye uchaguzi,

Pendekezo lingine ni kwamba kuwepo na kifungu cha 169 (4) ambapo Kikosi cha Polisi cha Uchaguzi kitaundwa kwa misingi ya uwiano wa Kijinsi yaani wanawake na wanaume hasa vijana wa kike na kiume.

Post a Comment

0 Comments