Rais wa Taasisi ya Utulivu Experience, Ibrahim Rwegerera akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la kutambua mchango wa viongozi waliofanya Tanzania kuwa na Amani na Utulivu kwenye Hoteli ya Hayatt Regecy The Kilimanjaro Hotel, jijini Dar es Salaam.
********
Taasisi ya Utulivu Space inampango wa kufanya uzinduzi wa Tamasha kubwa linalojulikana kama "Utulivu Experience" lenye dhima ya kuwaletea pamoja wananchi wa Kitanzania na Mataifa Mengine kwa ajili ya kufurahia Utulivu na Amani ambayo ni tunu ya Taifa tangu Tanzania ipate Uhuru.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Januari 30,2024 Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Ibrahim Rwegerera amesema kuwa uzinduzi wa Tamasha hilo utafanyika April 20 mwaka huu Bara Katika Ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini humo,lakini pia Tamasha hlio litafanyika Mwezi Novemba 20204 Visiwani Zanzibar.
Rwegerera ameongeza kuwa Tamasha hilo litawahusisha watu wa kada mbalimbali ikiwemo watu maarufu, viongozi na wenye matokeo chanya Ndani ya Jamii.
Aidha amesema kuwa wageni waalikwa katika tamasha hilo watapata fursa ya kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali ikiwemo wastaafu na wale waliosaidia katika kudumisha amani na mshikamano wa Taifa.
Amesema anaamini kuwa kupitia Tamasha hilo Tanzania itasherehekea faida za amani na Utulivu ambayo Moja ya alama inayolitambulisha taifa la Tanzania Duniani kote.
“Utulivu Experience ni jukwaa ambalo limetengenezwa kwa Neema za Mungu kufurahia amani na Utulivu wa Tanzania toka enzi za Wazee wetu ambao tunategemea kupata uzoefu wa njia walizotumia kudumisha amani ambayo mpaka leo tunayo” Amesema Rwegerera.
Hata hivyo amebainisha kuwa Tamasha hilo litakuwa na kiingilio kwa makundi matatu ambapo sehemu ya watu wa kawaida ni shilingi 270,000, VIP ni 1,350,000 na VVIP 2, 270,000.
Kwa upande wake Mshauri wa Tamasha hilo Antony Luvanda amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake na kuwaomba watanzania na raia wa nchi jirani kujumuika pamoja kuendelea kudumisha amani na Utulivu.
0 Comments