Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATUNUKIWA NISHANI YA MAPINDUZI YA VIONGOZI WENYE SIFA ZA KIPEKEE NA RAIS DKT. MWINYI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivalishwa Nishani ya Mapinduzi ya Viongozi wenye sifa za Kipekee (Order of Praise) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar tarehe 11 Januari, 2024. Rais Samia ametunukiwa Nishani hiyo katika kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kutunukiwa Nishani ya Mapinduzi ya Viongozi wenye sifa za Kipekee (Order of Praise) katika kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar tarehe 11 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya Utoaji wa Nishani iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu ya Zanzibar tarehe 11 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa hafla ya utoaji wa Nishani ya Mapinduzi ya Viongozi wenye sifa za Kipekee (Order of Praise) katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar tarehe 11 Januari, 2024.


Post a Comment

0 Comments