Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM YAWATAKA VIONGOZI KUWAWEKEA MAZINGIRA MAZURI WATU WENYE ULEMAVU


Na Emmanuel Mbatilo

KATIKA kuwainua watu wenye mahitaji maalum nchini ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Prof. William Anangisye amewataka viongozi mbalimbali kuweka mazingira mazuri ili yawe kichocheo kwao kutimiza malengo yao hususani kwenye sekta ya elimu.

Ameyasema hayo Prof. William Anangisye wakati wa maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ambapo tokea mwaka 1979 mpaka 2023 jumla ya wanafunzi takribani 621 katika nyanja mbalimbali za mafunzo na kati yao 457 wameshamaliza na 164 wanaendelea na masomo yao


Kwa upande wake Meneja wa CDS (CENTER FOR DISABILITY SERVICE) Dkt. Sarah Kisanga amesema Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kimejikita haswa kwenye elimu bora katika watu wenye mahitaji maalum ili kuweza kutokomeza umaskini na kuwa na afya bora ili kukabiliana na maendeleo endelevu.

Post a Comment

0 Comments