NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa mafunzo kwa Wanaharakati wa jinsia yenye lengo la kusaidia kuandika shuhuda zao kama kumbukumbu ya matokeo wanayo yapata wanapo kuwa kazini ili yatumike kuwafunza watu wengine.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo Desemba 27,2023,Mshauri Elekezi wa masuala ya Maendeleo, Tathimini na Ufatiliaji,Bw.Edson Nyingi amesema kuwa TGNP imeona kuna haja ya kuandika kuweka kumbukumbu nzuri na ya kudumu na kuachana na masimulizi pekee kwa njia ya mdomo ili kuweka kumbukumbu.
"Wadau wengi wa maendeleo wanafanya kazi na matokeo yanapatikana lakini hapakuwa na namna ya kuweka kumbukumbu za kudumu za matokeo ya kazi hizo hilo lilionekana swali huko mwanzoni na sasa hivi liko katika utekelezaji wa kazi za TGNP kuhakikisha inawajengea uwezo wadau wake kwa matokeo wa kazi wanazozifanya". Amesema Bw.Nyingi
Aidha ameeleza kuwa wanahitaji kuona matokeo ya kazi wanazofanya wadau wa TGNP ili kuona jitihada na harakati za kumkomboa mwanamke ili kuwa na usawa katika masuala ya mgawanyo wa rasilimali na umiliki wa mali.
"Hii Warsha imelenga katika kuwasaidia wadau kuweza kufatilia taarifa zinazotokana na hiyo mifumo inayoleta usawa,inayoleta uwiano,katika masuala ya kijinsia huko kwenye jamii wanakofanya kazi ili kuyafanya sio tu yawe katika kumbukumbu zao ili yatumike kuwaeleza wengine ili wajifunze kutokana na matokeo ya kazi zao". Ameeleza.
Amesema kuna matokeo sasa yanayoonekana kutokana na kazi za Wanaharakati wa jinsia wa TGNP sasa hivi wanaume wanaongozana na wake zao kwenda kliniki wanapokuwa wajawazito inatokana na harakati za TGNP za muda mrefu za kuleta usawa na uwiano wa majukumu katika familia.
Kwa upande wake, Mwanaharakati wa jinsia kutoka Mkoa wa Kilimanjaro shirika la Kisonge Community Development Organization Bi.Aika Manase ameishukuru taasisi ya TGNP kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo ynakwenda kusaidia kuweka kumbukumbu za kazi inayofanyika katika maandishi ambapo itachagiza kwa kiasi kikubwa kuweza kuishawishi serikali kuanzia ngazi ya jamii hadi serikali kuu kuhusiana na mambo yaliyojikita katika mlengo wa kijinsia.
"Kwa kweli ninalishukuru sana shirika la TGNP kwa kuandaa mafunzo haya yamekuja wakati sahihi sisi kama mashirika kwanza tulikuwa tunafanya kazi nzuri, tulikuwa tunawasimulia watu kwa njia ya mdomo, lakinj mafunzo haya yatatusaidia kama wadau wa maendeleo kuweka katika maandishi na kuweza kuishawishi serikali katika mambo yanayohusu Jinsia". Amesema
Bi.Aika amesema sababu ambayo imesababisha kipindi cha nyuma wasiweke kazi zao katika maandishi ni uelewa mdogo, ameeleza kwamba kutokana na mafunzo wanayopewa itawasaidia kuweza kuandika kumbukumbu hata inapotokea mdau wa jinsia amepoteza maisha wataweza kubaki wengine na kumbukumbu iliyopo kwa njia ya maandishi.
Naye Dereva Bajaji kutoka katika makundi yanayopigania Ukombozi,Haki na Usawa wa wanawake Bi.Husna Said ameeleza kuwa wamepata mafunzo ambayo yataweza kumsaidia kuandika hadithi kwa ajili ya kumbukumbu ya kazi ambayo ameifanya katika jamii ambayo itatumika kama chachu ya mabadiliko kwa watu wengine.
Mafunzo hayo yatakuwa kwa siku nne kuanzia leo Desemba 27-30,2023 ambapo yamehusisha, Mashirika,Makundi na watu wanaotetea Ukombozi,haki na usawa wa wanawake nchini.sisha, Mashirika,Makundi na watu wanaotetea Ukombozi,haki na usawa wa wanawake nchini.
0 Comments