Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KUFUATIA VIFO VYA WATU 47 WALIOFARIKI KWA MAFURIKO MANYARA

 



Na John Walter-Manyara

Juhudi za kuwaokoa watu waliokwama kwenye Matope zimeendelea Vijiji vya Katesh na Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara baada ya Mafuriko kuyakumba maeneo hayo na kusababisha vifo vya watu 47 na wengine 85 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga watu zaidi wanahofiwa kufukiwa na matope baada nyumba na makazi yao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo kutoka Mlima Hanang’.

Eneo kubwa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi na Katesh ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya ya Hanang’.

Nyumba za watu zimezingirwa na mafuriko na miti iliyosombwa na mafuriko kutoka sehemu ya Mlima Hanang yamesababisha barabara ya Katesh kwenda Singida kushindwa kupitika kwa muda.
Wakazi wa Hanang’ wamesema hawajawahi kushuhudia hali kama hiyo na kwamba kwao hilo ni janga kubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia tukio hilo na kuzitaka mamlaka zote zihamishie nguvu wilayani Hanang kutoa msaada wa haraka.

Post a Comment

0 Comments