Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Salum Kalli leo tarehe 2 Desemba, 2023 wameongoza mbio na matembezi ya furaha pamoja michezo mbalimbali mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya shukrani kwa Mlipakodi ambayo imeandaliwa na ofisi ya TRA Mkoa wa Kigoma.
0 Comments