Ticker

6/recent/ticker-posts

KIPINDUPINDU CHAUA WATU WANNE KAGERA


Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa 

Na Mariam Kagenda - Kagera
Watu wanne wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu katika wilaya ya Missenye Mkoa wa Kagera. 

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa amesema kuwa ugonjwa huo umegundulika katika wilaya ya Missenye kata ya Bugorora kijiji cha Buchurago.

Mwassa amesema kuwa watu wanne wamefariki, watu wanne wamelazwa hospitali ya St. Tereza wilaya ya Missenye wakiendelea na matibabu na wengine watatu wametibiwa na kuruhusiwa.

Amesema kuwa kila mmoja anatakiwa kuchukua tahadhari kubwa na kuepuka safari zisizo za lazima kwani ugonjwa huo ni hatari na unaambukizwa kwa haraka ambapo mkoa huo unaendelea na uchunguzi na kufuatilia watu wote waliochangamana na wagonjwa wakati wakiugua au wakati wa mazishi.

Aidha amesema kuwa pia katika kisiwa cha Goziba kuna mtu mmoja amefariki dunia na kabla ya kufariki kinyesi chake kilifanana na ugonjwa wa kipindupindu baada ya kuchukuliwa Sampuli ingawa bado haijadhibitika hivyo wanaendelea na uchunguzi.

Post a Comment

0 Comments