NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMPUNI inayojishughulisha na mambo ya ujezi ya Derm Group, imeadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini, huku ikijivunia mfanikio makubwa waliyoyapata katika shughuli yao hiyo.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Desemba 16, 2023 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi wote wa kampuni hiyo, pia yalihusisha wadau mbalimbali, huku Mgeni Rasmi, akiwa ni Mkuu wa Mkoa (RC) wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Chalamila aliipongeza Derm Group kwa mafanikio hayo, huku akiiahidi sapoti ya hali ya juu kutoka kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
“Miaka 25 si mchezo, niwapongeze sana uongozi na wafanyakazi wote wa Derm Group kwa leo hii kuadhimisha miaka 25 tangu mlipoanza shughuli zenu hapa nchini.
“Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, siku zote imekuwa bega kwa bega na sekta binafsi ambazo zimekuwa zikishirika kwa namna nyingine katika ujezi wa Taifa letu kwa kutoa ajira kwa Watanzania na ushalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali.
“Niwahakikishie Serikali ya Rais wetu mwenye uchungu wa dhati kabisa na maendeleo ya nchi yetu na anayegushwa na matatizo ya watanzania, ipo tayari kutoa ushirikiano wowote mtakaouhitaji ili kuendeleza gurudumu la maendeleo ya nch9i yetu,” alisema RC Chalamila.
Aliwataka wafanyakazi wa Derm Group kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa yao yote ili kuzidi kuipaisha kampuni hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Derm Group, Ridhuan Mringo, alisema“Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufikisha umri huu wa miaka 25 toka tumeanza shughuli zetu hapa nchini.
“Mafanikio haya hayajaja hivi hivi, bali yametokana na mipango na mikakati thabiti ya uongozi kwa kushirikiana na wafanyakazi wetu wote ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa,” alisema.
Mringo alisema kuwa pia Serikali za awamu zote tangu walipoanza shughuli zao, zimekuwa zikiwapa ushirikiano mkubwa, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kukua kiwa kampuni yao.
“Nitoe pongezi za dhati kabisa kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk, Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ilivyochangia kwa kisi kikubwa kukua kwa kampuni yetu ndani ya miaka hii michache tangu Mama yetu aliposhika madaraka.
“Kwa kweli tumepiga hatua kubwa sana kutokana na jinsi Serikali ilivyotujengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zetu hapa nchini bila wasi wasi wowote. Tunamshukuru sana Mama yetu Samia Suluhu Hassan,” alisema Mringo.
Alisema kuwa kampuni yao iliyoanza mwaka 1998, imefanikiwa kutoa ajira ya kudumu kwa zaidi ya Watanzania 500, wakiwa ni wanaume na wanawake, wanaohusika katika nyanja zote za shughuli zao.
Derm Group ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama Derm Electrics (T), ni kampuni kubwa inayokua kwa kasi ikimilikiwa na Mtanzania, yenye sifa dhabiti ya utendaji kazi wa kitaalamu kutokana na kuwa na wafanyakazi wabobevu na uongozi thabiti.
Kampuni hiyo imekuwa ikijishughulisha na ubunifu, ufungaji na matengenezo ya nyaya za umeme na mifumo yake, ufungaji wa transfoma za usambazaji na uunganishaji wa wateja wapya katika maeneo ya vijijini ambayo hayana umeme.
Kwa zaidi ya miaka 25, Kampuni ya Derm Group imekuwa ikishiriki katika miradi mingi mikuu ya ujenzi na uhandisi, hivyo kupata uzoefu na sifa kama mmoja wa wakandarasi wakuu wa umeme nchini Tanzania.
0 Comments