CHAMA cha Siasa Cha Kijamii (CCK) wamezindua sera ya kijinsia ikiwa na lengo la kuleta usawa kwa Taifa katika kuwapata viongozi wenye kuleta tija kwa Taifa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa unatarajia kufanyika mwaka 2024 pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Kijinsia, Mwenyekiti wa Taifa Chama Cha UPDP, Twalib Kadege na mgeni rasmi katika hafla hiyo, amesema kuwa sera hiyo inahimiza uongozi unaozingatia usawa wa kijinsia ambao unaleta maendeleo chanya katika jamii kama anavyofanya Rais Dkt. Samia Suruhu Hassani kwani jitaidi zake zimekuwa na manufaa kwa wote.
Amesema kuwa sera hiyo itasaidia utasaidia kuwaamsha wenye uhitaji maalum kushiriki kwa wingi sawa na wanaume kwenye harakati za kisiasa kwa kuona sasa kuna sera inayowalinda na wao kupata nafasi kubwa za kiuongozi.
Mwenyekiti wa Chama cha Siasa Cha Kijamii (CCK) David Mwaijojele, amesema kuwa sera ya kijinsia italeta ahueni katika kuhakikisha changamoto mbalimbali zinapatiwa majibu kupitia mikakati ambayo inampa fursa mwanamke kugombea na kupata nafasi katika ngazi mbalimbali.
Amesema kuwa mchakato huo wa uandishi wa sera ya Kijinsia ulifanyika septemba 2022 kufuatia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na baraza la vyama vya siasa sambamba na mashirika mbalimbali yakiwemo la TGNP,Wildaf,Ulingo kukaa na kuunga mkono suala la vyama vya siasa kuunda sera ya ushiriki wa wanawake na makundi maalum.
‘Haya ndio matunda tunayoyaona kwani kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala kuhusu wanawake na makundi maalum kushiriki katika nafasi mbalimbali hivyo tunaizundua sera hii na itaendelea kutumika kati ngazi ya chama kwa kupigania chapuo wanawake kupata nafasi katika suala la uongozi’amesema Mwenyekiti Mwaijolele
Nae Mwenyekiti wa Bodi Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali, amesema kuwa wanawake wanauwezo wa kufanya mambo makubwa kama wakipewa nafasi katika uongozi, hivyo sera hiyo itakuwa ni rafiki katika kufikia malengo.
Akilimali amepongeza hatua hiyo ya sera za jinsia kukubalika katika vyama vya siasa kwani wamefanyia kazi kwa muda mrefu katika kujenga usawa kwenye nyanja mbalimbali.
‘Tuelewe kabisa suala la jinsia ni mahusiano katika jamii ambayo yanadai kuwa na usawa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uongozi au hata katika kumiliki rasilimali lakini tunachukua kiini cha uongozi’amesema Mama Akilimali
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji WILDAF Anna Kulaya amewasisitiza wanachama wa CCK kuisoma sera hiyo na kuielewa ili wafahamu wanawajibu gani wa kuitekeleza kwa ufasaha
Hata hivyo Vyama vya Siasa Nchini vimetakiwa kuwa na sera ya Jinsia katika vyama vyao Lengo likiwa ni kuhakikisha vyama vinafanya michakato yake ya ndani na kuandaa viongozi wa kitaifa kulingana na usawa wa jinsia
Katika Mkutando wa uzinduzi wa sera ya kijinsia sambamba na uchaguzi Mkuu wa chama hicho umehudhuriwa na wanachama na wadau mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.
0 Comments