Muonekano wa mizinga ya kisasa ambayo wafuga nyuki wamepatiwa.
Mhifadhi Misitu na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Kahama Martha Machibya (katikati kushoto) akikabidhi mizinga ya kisasa iliyotolewa na Barrick Buzwagi kwa Katibu wa kikundi cha wafuga nyuki, Rehema Juma.
Mhifadhi Misitu na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Kahama Martha Machibya (kushoto) akikabidhi funguo za pikipiki ya kubebea mizigo iliyotolewa na Barrick Buzwagi kwa Katibu wa kikundi cha wafuga nyuki,Rehema Juma.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii (Community Relations Manager) wa Barrick Buzwagi,Stanley Joseph,akiongea katika hafla hiyo.
Mhifadhi Misitu na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Kahama Martha Machibya (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick Buzwagi katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na Maofisa wa Barrick Buzwagi na baadhi ya wanakikundi waliokabidhiwa msaada.
***
Katika mwendelezo wake wa kuwawezesha wakazi wa maeneo yaliyopo jirani na Mgodi wa Barrick Buzwagi, kuwa endelevu baada ya mgodi huo ambao uko katika mchakato wa kufungwa, umekabidhi Ofisi, Kiwanda na Vifaa mbalimbali kwaajili ya shughuli ya ufugaji wa nyuki pamoja na uviunaji wa asali katika kikundi cha Umoja wa ufugaji nyuki kilichopo katika kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi mradi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii (Community Relations Manager) wa Mgodi huo aliyemwakilisha Meneja wa Mgodi huo, Stanley Joseph, amesema ufadhili wa kikundi hicho ulianza cha wafugaji wa nyuki ulianza mwaka 2010 ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 300 zimetumika katika matumizi mbalimbali ya vifaa vya kisasa vya kuwezesha ufugaji bora na kununua ekari 6 za misitu kwa ajili ya kuwa na eneo la kutosha la kuendeshea mradi huo.
Joseph, amesema katika awamu hii ya ufadhili katika uboreshaji zaidi wa mradi wameongeza mizinga 50 ya kisasa, pikipiki ya kusaidia kubebea mizigo pamoja na mashine za kisasa 17 za kuchakata asali.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mhifadhi Misitu na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Kahama Martha Machibya, ameipongeza Barrick Buzwagi, kwa kuendelea kuwezesha wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mgodi huo licha ya kuwa haufanyi shughuli zozote za uzalishaji.
Machibya, amewaasa Wanakikundi hao kutumia vyema Rasilimali hizo kuweletea maendeleo na siyo kuleta malumbano kwani hawataona faida ya kikundi hicho pia amewataka wananchi kulinda mazingira na kuheshimu maeneo ambayo yametengwa kama hifadhi na serikali kwani yanamsaidia kila mmoja akitolea mfano kwa kikundi hicho cha umoja wa wafuga nyuki Mwendakulima.
Naye Katibu wa kikundi hicho, Rehema Juma, akiongea kwa niaba ya wenzake baada ya kupokea vifaa pamoja na ofisi ya kisasa, ameushukuru Mgodi wa Barrick Buzwagi na kuahidi kuwa watautumia mradi huo kwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wanafahamu fursa zinazopatikana kupitia ufugaji wa nyuki licha ya kuvuna asali pia ni kuwa kuna soko kubwa duniani la sumu ya nyuki.
0 Comments