Ticker

6/recent/ticker-posts

WORLD VISION TANZANIA YAZINDUA MRADI WA GROW - ENRICH KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO SHINYANGA


Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI katika wilaya za Shinyanga Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen wakikata keki wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Shirika la World Vision Tanzania limezindua Mradi wa GROW-ENRICH (Enhancing Nutrition Services to Improve Maternal and Child Health) unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto katika wilaya za Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga.


Uzinduzi huo uliohudhuriwa na Viongozi mbalimbali na Maafisa wa Serikali umefanyika leo Jumatano Novemba 1,2023 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Samizi amelipongeza shirika la World Vision Tanzania kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali inayoendana na vipaumbele vya Serikali hususani ujenzi wa miundombinu ya afya, elimu, maji, lishe na afua za uimarishaji wa uchumi wa kaya kwa wananchi wenye hali duni ya kipato.


Amesema mradi huo utakaotekelezwa kwa muda miaka mitano utaenda kutatua changamoto za lishe kwa makundi maalumu yanayolengwa. Mradi huo utafanya kazi katika nyanja za afya, lishe, kilimo, kuimarisha uchumi wa kaya na masuala ya usawa wa kijinsia.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen na Mkurugenzi wa Miradi World Vision Tanzania Bi. Nesserian Mollel (kulia)  wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH

“Kwa kipekee nilishukuru Shirika la World Vision na Serikali ya Ujerumani kwa kutupatia mradi huu wa GROW-ENRICH hapa Shinyanga, tunawashukuru sana, mngeweza kuupeleka sehemu nyingine maana uhitaji ni mwingi hata sehemu nyingine lakini mkaupa mkoa wetu kipaumbele. Sisi kama serikali tunatoa na tutatoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa juhudi hizi zinafikia malengo yake kwa ufanisi”,amesema Samizi.

Ameeleza kuwa ili jamii iweze kunufaika na uwepo wa mradi huu ni lazima serikali kupitia viongozi ngazi zote wawaandae wananchi katika vijiji vitakavyohudumiwa na mradi kuwa tayari kujitokeza kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.

“Nitoe wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa ajili ya kushiriki kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huu wa GROW-ENRICH ili tuweze kupunguza na ikiwezekana kufuta kabisa vifo vya mama na mtoto”, ameongeza Samizi.

Aidha Samizi amewaagiza watumishi wa serikali wanaohusika moja kwa moja na mradi huo kuhahikikisha mradi unaleta matokeo chanya, kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Shirika la World vision Tanzania katika utekelezaji wa shughuli za mradi na hategemei kuona mtu yeyote atakayekwamisha.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya taifa letu na ni moja ya eneo la kipaumbele cha kimaendeleo. Uwepo wetu sote katika uzinduzi huu unaendelea kuonesha umuhimu wa kuimarisha ushiriki wa kila sekta, yaani Serikali na wadau wetu World Vision na Kivulini na wananchi kwa ujumla”, amesema.

Amebainisha kuwa mapambano dhidi ya vifo vya mama na mtoto yanaweza kufanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo kuboresha na kuhamasisha ulaji wa vyakula vyenye viini lishe kwa wanajamii, kuboresha huduma za afya na kuielimisha kaya na jamii nzima juu ya umuhimu wa lishe bora na afya kwa mama na mtoto.

Njia zingine za kupambana na vifo vya mama na mtoto ni pamoja na kuelimisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia na kuwajengea msingi bora wa elimu ya masuala ya uzazi na lishe kwa vijana wa kike na wa kiume ili kuwatayarisha kuwa wazazi bora na pia kuwawezesha vijana kuzitambua changamoto za masuala ya lishe na uzazi namna wanavyoweza kuzitatua.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen amesema mbali na kuzindua mradi wa GROW- ENRICH pia wamepitia malengo ya mradi na matokeo tarajiwa ya mradi katika kata za Mwakipoya, Shagihilu na Malwilo wilayani Kishapu na kata za Iselamagazi, Pandagichiza, Mwalukwa, Itwangi, Samuye na Usanda katika wilaya ya Shinyanga.


“Mradi huu Unatekelezwa na World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI katika kata 9, vijiji. 20 katika wilaya za Kishapu na Shinyanga. Lengo kuu la mradi ni kuchangia katika kupunguza vifo vya mama na mtoto katika maeneo yaliyolengwa na mradi ambapo wanawake ni wanufaika wa moja kwa moja wa huduma ya mama na mtoto”,ameeleza Dkt. Cohen.

Amesema wanatarajia kuwa mradi huo utachangia kupungua kwa vifo vya mama na mtoto katika kaya na jamii zilizo hatarini.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI katika wilaya za Shinyanga Kishapu Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Novemba 1,2023
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI katika wilaya za Shinyanga Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI katika wilaya za Shinyanga Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania na Shirika la KIVULINI katika wilaya za Shinyanga Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen wakijiandaa kukata keki wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Keki maalum wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen wakikata keki wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
 Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Kishapu  Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) akimlisha keki  Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali na miradi World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Picha za kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Picha za kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Picha za kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Picha za kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Picha za kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Picha za kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH
Picha za kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Mradi wa GROW-ENRICH

Post a Comment

0 Comments