Washiriki na wadau wa maendeleo Mkoa wa Tanga wakifuatilia kongamano.
*********************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.
IMEELEZWA kwamba uwekezaji mkubwa unaofanywa katika Mkoa wa Tanga utawezekana kwa kiasi kikubwa endapo huduma za kifedha zitakuwepo kwa ukubwa wake na kila wakati.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus ameyasema wakati wa kongamano la uwekezaji, biashara na utalii na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Tanga ambapo pia aliwataka wawekezaji kutumia benki hiyo kwa ajili ya mikopo.
"Sisi hapa Tanga tunayo matawi zaidi ya 12 kwa Wilaya zote 8, kwa maana kuna baadhi ya Wilaya tuna matawi mawili mawili, hii itarahisisha upatikanaji wa huduma hizi za kifedha ambazo tunaziongelea" alisema.
"Lakini itoshe tu kusema NMB imejipanga na itaendelea kushirikiana na serikali katika kuchagiza maendeleo muhimu ya nchi yetu" amebainisha Ladislaus.
Aidha ameeleza kwamba NMB ina uwezo mkubwa wa kuhudumia sekta mbalimbali za uwekezaji ambapo wameanza kwa uzoefu wa kuhudumia sekta ndogo ndogo na kati kwauwa na muda mrefu wa kuwahudumia.
"Benki ya NMB imeendelea kukuza mtaji wake, na sasa niwaambie wawekezaji wakubwa na wa kati kwamba benki ina uwezo mkubwa wa kutoa mitaji ambayo itachagiza uwekezaji huu tunaoungelea hivi sasa, kwa taarifa tu, uwekezaji mkubwa unaweza kuchukua mkopo hadi sh bilioni 340" amesema.
0 Comments