Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Muheshimiwa Kassim Majaliwa ametoa agizo kwa Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI kukamilisha kwa haraka taratibu za utoaji wa mikopo ya asilimia kumi wa wajasiriamali na ifikapo 15/1/2024, taarifa zote ziwe zimetolewa ili halmashauri ziruhusiwe kuanza kutoa mikopo hiyo.
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa yenye kauli mbiu Elimu ya fedha, msingi wa maendeleo ya kiuchumi , yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Aidha baadi ya maagizo aliyotoa Waziri Mkuu Majaliwa katika hotuba yake kwa Wizara ya fedha ni pamoja na Wizara ya fedha kuendelea kusimamia na kuratibu utekekezaji wa fedha kwa kutoa elimu endelevu ya fedha kwa umma mjini mpka vijijini huku wakishirikiana na watu wa taasisi za fedha.
Amesema kuwa Wizara iendelee na mpango maalum wa kutoa hamasa ili kila mwananchi atumie njia rasmi za huduma ya fedha ikiwemo suala la wananchi kudaibrisiti wanapopata huduma, akiendelea kutoa maagizo kwa Wizara ya Fedha Majaliwa amesisitiza Wizara kuendelea kuratibu kwa watoa huduma wote wa kifedha kupunguza gharama ya huduma wananzozitoa ikiwemo suala la riba katika mikopo, ada na mengineyo.
Sambamba na hayo yote Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza Wizara kuimarisha mifumo ya kuwalinda watumiaji wa fedha kwa kutoa elimu kwa wannchi kabla ya kufunga mikataba ya mikopo, lakini pia Wizara kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki maonyesho na kupa elimu ya fedha.
Maonyesho ya Wiki ya huduma za fedha Kitaifa yameanza tarehe 20/11/2023 na kumalizika tarehe 26/11/2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
0 Comments