Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKENDA MGENI RASMI MAONESHO YA KITAIFA YA GUNDUZI NA TAFITI ZINAZOFANYWA NA WANAFUNZI VYUONI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya Kitaifa ya kazi za ugunduzi na tafiti zinazofanywa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini ambayo yatafanyika Desemba 5,2023 kwenye ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 26,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi mwenza wa Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST) Dkt Gozibert Kamugisha amesema kuwa YST imekuwa ikitoa fursa kwa vijana kupatiwa mafunzo ya mbinu za kiutafiti wa sayansi, kufanya utafiti wa kisayansi, na kufanya maonyesho ya gudunzi zao baada ya mchakato mrefu wa kiutafiti.

"Tofauti na miaka iliyopita, mwaka huu kuna ongezeko kubwa kwa idadi ya gunduzi ambazo ziko katika mfumo wa Artificial Intelligence (AL). Hii ni ishara kuwa vijana wetu wanaenda na kasi ya dunia ya sasa ambayo inashuhudia ongezeko kubwa la gunduzi zenye kutumia AL na matumizi yake". Amesema

Aidha amebainisha kuwa maonyesho hayo yatashirikisha wanafunzi 90 ambao wataonesha gunduzi mbalimbali zinazohusisha matumizi ya akili bandia ikiwa ni pamoja na mifumo ya umwagiliaji katika mashamba, mifumo ya kuzuia magonjwa kwa mimea pamoja na mifumo ya kusaidia kutunza mazingira.

Aidha amesema kuwa mwaka huu wanafunzi walituma maombi ya gunduzi 979 wakiomba fursa ya kushiriki katika program ya YST, na baada ya kufanya mchujo, maombi 361 yalichaguliwa na wanafunzi wakapatiwa mafunzo ya namna ya kuendeleza kazi zao za kisayansi.

Pamoja na hayo amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuunga mkono na kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya kitaifa ya kazi za ugunduzi na tafiti zinazofanywa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini hali itakayoziwezesha gunduzi hizo kuleta tija katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Bi. Caren Rowland amesema kuwa taasisi hiyo imeendelea kuboresha program mbalimbali zinazolenga kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao ambapo mpaka sasa imeshadhamini wanafunzi 41 katika mikopo ya elimu ya juu na wanatarajia kudhamini wengine wanne na hivyo kufikia wanafunzi 45.

Nao baadhi ya wanafunzi waliowahi kushiriki mashindano hayo wamesema mafunzo hayo yaliwawezesha kuendeleza tafiti zao na hivyo kufikia maleongo yao na hivyo kuongeza mchango wao katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii

Post a Comment

0 Comments