Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) , Prof. William Pallangyo, akihutubia katika Mahafali ya 21 ya Taasisi hiyo Kampasi ya Singida yaliyofanyika Novemba 17, 2023.
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imewataka wahitimu katika taasisi hiyo watakaopata ajira serikalini kwenda kusaidia kupunguza matatizo ambayo yamekuwa yakiibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG) katika kaguzi anazozifanya hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na TIA, Wakili Said Chiguma,alisema hayo Novemba 17, 2023 wakati wa mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Singida ambayo wahitimu 1700 walitunikiwa vyeti baada ya kuhitimu fani za uhasibu,raslimali watu, ununuzi wa umma na usimamizi wa biashara.
Alisema wahitimu watakaopata ajira wakajiepushe na vitendo ambavyo ni kinyume na kanuni za maadili ya taaluma zao ambavyo vinaweza kuwasababisha kupoteza ajira, heshima na hata kufungwa jela.
“Kutokana na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) kama ambayo ameibua matatizo mbalimbali, ninyi mtakaopata ajira serikalini muende kupunguza au kutoa matatizo hayo na sio kuyatengeneza, “ alisema.
Chiguma alisema wahitimu hao wanatakiwa kufahamu kuwa jamii na taifa kwa ujumla wanategemea kuona ujuzi walioupata unawapa fursa mbalimbali za kiuchumi, biashara na kutengeneza ajira ambazo zitawanufasha jamii.
Alisema TIA imeendelea kuwa kinara katika kuwanoa wahitimu wake ambao wanafanya vizuri katika soko hususani mitihani ya Bodi ya Wahasibu na wakaguzi wa Maheabu (NBAA) na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ambapo wahitimu wa TIA waliibuka katika nafasi ya tano bora kati ya vyuo na taasisi zaidi ya 20.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo, alisema kiumekuwa na ongezo kubwa la wanafunzi wanaojiunga katika taasisi hiyo kila mwaka wa masomo kutokana na ubora wa elimu inayotolewa unaotokana na mitaala inayowajenga wanachuo wa ngazi zote msingi wa umahiri na hivyo kumwezesha mhitimu kuajiriwa na kujiari anapohitimu masomo yake.
Alisema sababu nyingine ya kuwepo na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga TIA ni kutokana na utaratibu mzuri wa serikali wa kuwapangia vyuo moja kwa moja wahiyimu wa kidato channe waliofaulu nakukidhi vigezo kupitia TAMISEMI na ongezeko la mikopo kwa wanafunzi wa kozi za shahada.
“Katika suala la mikopo katika mwaka huu 2023/2024 serikali imepanga kuwafadhiliwanachuo 810 wa shahada katika kampasi hii ya Singida, hili ni ongezeko la asilimia 15.9 ukilinganisha na anachuo 699 waliofadhiliwa mwaka 2022/2023,”alisema.
Prof.Pallangyo alisema katika kuhakikisha wanachuo wanapata ujuzi na kitaaluma, TIA kampasi ya Singida inawapa fursa ya kujifunza kwa vitendo na kuunga mkono juhudi zao katika mawazo yao ya biashara na uwekezaji hali ambayo imewasaidia kuongezeka kwa biashara zao na kukua.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba katika mahafali hayo alisema serikali ina mpango wa kukuza diplomasia ya uchumi hivyo mafunzo wanayopata wahitimu wa TIA yaendane na shabaha ya Rais Samia Suluhu Hassani.
Mgeni rasmi wa mahafali hayo Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleimani Mwenda (katikati) ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akiwasili kwenye mahafali hayo kwa maandamano maalumu
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na TIA, Wakili Said Chiguma (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) , Prof. William Pallangyo wakimpokea Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleimani Mwenda alipowasili kwenye mahafali hayo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba.
Wahitimu wa Shahada ya Uhasibu wakionesha furaha zao wakati wa mahafali hayo.
Mahafali yakiendeleaMgeni rasmi wa mahafali hayo Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleimani Mwenda akiyaahirisha mahafali hayo ya 21 ya mwaka 2023.
Mahafali yakiendelea. Kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa TIA, Dkt. Momole Kasambala, Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala TIA, Dkt. Issaya Hassanal ,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko TIA, Lilian Rugaitika na Mshereheshaji wa mahafali hayo, Daudi Mashauri.
Wazazi, Walezi na ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo. Kutoka kulia ni Viongozi wa TIA wakishiriki mahafali hayo. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Ushauri, Mystica Ngongi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo (NDC) ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Ushauri Nicolaus Shombe Mjumbe wa Bodi ya Ushauri na Mhadhiri Mwandamizi-Chuo Kikuu cha Mzumbe, Leonada Mwagike na Mkurugenzi wa Utawala, Menejiment na Usimamizi wa Rasilimaliwatu-Ofisi ya Rais TAMISEMI, Emma Lyimo.
Wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Biashara wa TIA Singida wakiwa wameweka kofia zao begani wakati wakitunukiwa vyeti vyao.
Wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wakitunukiwa vyeti vyao.Wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wakionesha furaha zao baada ya kutunukiwa vyeti vyao.
Mahafali hayo yakiendelea.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TIA.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao.
0 Comments