Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU WATAKIWA KUTUMIA MBINU ZA KITAALUMA KUKABILIANA NA UTUMWA WA KISASA

WADAU nchini wametakiwa kutumia mbinu za kitaaluma zinazotokana na tafiti mbalimbali zinazofanywa katika kukabiliana na utumwa wa kisasa na usafirishaji haramu wa binadamu hali itakayosaidia kuepuka madhara yake kiuchumi pamoja na kijamii.

Rai hiyo imetolewa hii leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Albert Chalamila wakati akizindua Kongamano la kimataifa linalolenga kujadili athari za utumwa wa zamani katika historia ya Afrika ya kisasa lililoandaliwa na Idara ya historia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam lengo likiwa kujafili athari za utumwa katika maisha ya sasa barani Afrika.

Vilevile ameeleza kuwa bado kumekuwa na matukio kadhaa yanayohusisha utumwa na usafirishaji haramu bmwa binadamu hususa ni katika mkoa wa dar es salaam ambapo ameweka wazi kuwa jiji hilo limejidhatiti kukomesha suala hilo ikiwa ni pamoja na kutumia mapendekezo yatakayotokana na kongamano hilo.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi idara ya historia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo Dkt. Salvatory Nyanto amesema kongamano hilo limelenga kuja na njia za kukomesha utumwa wa kisasa ikiwa ni pamoja na kufanya majadiliano yatakayowezesha utungwaji wa sera na miongozo ya kukomesha biashara hiyo.

Post a Comment

0 Comments