Ticker

6/recent/ticker-posts

UECO YATOA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA TAULO ZA KIKE ZA KUFUA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MKUNDI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Unganisha Environmental Conservation Organization (UECO), Sophia Kalinga akionesha taulo ya kike ya kufua
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Unganisha Environmental Conservation Organization (UECO), Sophia Kalinga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mkundi Mlimani manispaa ya Morogoro.


****


Shirika la Unganisha Environmental Conservation Organization (UECO) limetoa mafunzo ya Ufundi stadi ya utengenezaji wa taulo za kike (pedi) za kufua katika shule ya sekondari Mkundi Mlimani manispaa ya Morogoro ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutunza mazingira.





Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Unganisha Environmental Conservation Organization (UECO), Sophia Kalinga amesema wametoa mafunzo hayo baada ya kuona changamoto wanazokutana nazo mabinti wanapotumia pedi zisizofuliwa ikiwa ni pamoja na kukosa vifaa rafiki vya kutupia pedi hizo lakini pia kwa ajili ya usalama wa afya zao.


Pia UECO imepeleka miti ya matunda na kuwapa elimu ya Utunzaji na uhifadhi wa Mazingira.

Post a Comment

0 Comments