Ticker

6/recent/ticker-posts

TUELEKEZE JUHUDI ZETU KWENYE AFYA NA MALEZI YA WATOTO NJITI - BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko ameitaka Jamii, Wadau na Serikali kwa ujumla kuelekeza nguvu na juhudi katika kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya Wakati.

Ameyasema hayo jana kwenye Hotuba iliyosomwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima kwenye Hafla ya Kusherekehea Mafanikio ya Ajenda ya Mtoto Njiti 2021 iliyowashirikisha Mawaziri, wabunge, Wawakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali na Wawakilishi wa Taasisi za Taifa za Afya, Elimu, Kazi, Maendeleo ya Jamii na Sheria kutoka taasisi mbalimbali Novemba 07, 2023 Jijini Dodoma.

"Dunia inatualika sote tuelekeze juhudi zetu kwenye afya na malezi ya watoto njiti. Tunaalikwa kusikiliza kwa huruma vilio vya mamilioni ya akina mama na akina baba wanaolazimika kurudi kazini ilihali wakiwa na watoto njiti. Tunaishukuru sana Doris Mollel Foundation kwa kuchukua jukumu la kutatua changamoto hii katika kupigania maisha ya watoto njiti.

Kwa niaba ya Serikali, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Doris Mollel Foundation, ambayo kimsingi inafanya kazi ya kunuru maisha ya watoto njiti kwa kama kufanya hivi leo, ambapo tunaalikwa kwa mara nyingine kuangalia namna bora tunayoweza kutatua changamoto ya Maisha ya watoto njiti nchini Tanzania. Juhudi zenu, hazithaminiwi ndani tu, bali hata nje kwa vile sasa tunaishi kwenye zama za utandawazi." Dkt. Dotto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Post a Comment

0 Comments