Ticker

6/recent/ticker-posts

TANESCO YAKUTANA NA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limefanya kikao na Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuimarisha mahusiano na mawasiliano ili kupunguza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Kikao hicho chenye kauli mbiu ‘TANESCO Yetu, Umeme Wetu, Njoo Tuzungumze’ kimefanyika leo Jumatano Novemba 15,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

Katika kikao hicho, Waheshimiwa Madiwani wameeleza changamoto walizonazo kwenye maeneo yao pamoja na vipaumbele vya maeneo yanayopaswa kupatiwa huduma ya umeme.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameipongeza TANESCO kwa kufungua milango ya kukutana na Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi akibainisha kuwa mazungumzo yanaleta hitimisho la mambo yote.

“Kauli mbiu hii ya TANESCO Yetu, Umeme Wetu, Njoo Tuzungumze ni nzuri kwani, hitimisho la mambo yote ni mazungumzo, njoo tuzungumze inatoa fursa kwa Waheshimiwa Madiwani kueleza changamoto na vipaumbele kwenye kata zao, kikao hiki kiwe chachu ya mahusiano na mawasiliano baina ya Madiwani na TANESCO,hakikisheni mnawasiliana ili kupata ufumbuzi wa changamoto zinazojitokeza”,amesema Mhe. Samizi.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyotoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya umeme.

“Serikali ya awamu ya sita inaupiga mwingi, sisi Serikali na TANESCO tumekubaliana kuwa ifikapo mwezi Februari mwaka 2024 kila Kijiji kipate huduma ya umeme. Hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwani ilani imeelekeza wananchi wanapatiwe huduma ya umeme”, amesema.

“Ni lazima tutambue kuwa Umeme siyo anasa bali umeme ni huduma ya msingi katika ulimwengu huu wa sasa. Umeme ni Maisha, umeme ni uchumi hivyo ni lazima wananchi wapate huduma ya umeme. Na tunapopeleka huduma za umeme ni vyema pia tuyatambue maeneo yenye huduma za kijamii mfano zahanati na shule”,ameongeza Mhe. Samizi.

Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi ya umeme katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga ikiwemo miradi ya REA na Mradi wa mkubwa Umeme Jua wilayani Kishapu huku akiwatoa hofu wananchi kuwa itaendelea kuyafikia maeneo yenye changamoto ili kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na huduma ya umeme.

“Tumekutana na Waheshimiwa Madiwani ili tuzungumze. Mhe. Diwani kama una shida usiilaze, piga simu muda wowote tutatoa ufafanuzi kuhusu changamoto yoyote. Naomba madiwani wote muwe na simu zangu (Meneja Tanesco Mkoa) , simu za Afisa Uhusiano na Mainjinia wa wilaya ambao mtawasiliana nao kuhusu mahitaji mbalimbali ili yapate ufumbuzi”,amesema Mhandisi Mwakatobe.

"Ni vizuri tukawa na mawasiliano, tuzungumze yanayotukabili ili tuyatatue. Madiwani mtatusaidia kutoa ufafanuzi kwa wananchi. Serikali inatoa fedha kila mwaka kwa ajili ya kusambaza umeme,naomba Waheshimiwa madiwani mfanye kazi kwa ushirikiano na TANESCO ili kutimiza malengo ya serikali ya kuhakikisha kila Kijiji kinafikiwa na huduma ya umeme",ameongeza.

Akizungumzia kuhusu tahadhari ya Mvua kubwa za El Nino, Mhandisi Mwakatobe amesema TANESCO inaendelea kukarabati miundombinu ya umeme ikiwemo kuweka nguzo na kuondoa miti iliyopo kwenye njia za umeme.

"Nguzo za miti nyingi zimeoza hali inayosababisha umeme ukatike pindi nguzo zinapoinama na kugusana,. Tunaendelea kubadilisha nguzo na tunasubiri kupata nguzo za zege ili kutatua changamoto kwenye maeneo yenye changamoto mfano maeneo yenye maji",ameeleza.

Nao Madiwani walioshiriki kikao hicho licha ya kueleza changamoto na vipaumbele kwenye maeneo yao pia wamempongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa kuandaa kikao hicho ambao kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mahusiano na mawasiliano baina ya Madiwani na TANESCO ili wananchi wapate huduma ya umeme.

Aidha Madiwani hao wameomba baadhi ya maeneo Mjini Shinyanga ambayo hayana huduma ya umeme hususani yenye sifa za vijiji  yaunganishiwe umeme kwa mfumo wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kulipia shilingi 27,000/= kama wanavyopewa wananchi waliopo vijijini kwani wengi wao hawana uwezo wa kumudu gharama kwa mfumo wa gharama zinazotozwa kwa wananchi wa Mjini.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumatano Novemba 15,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini

Kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Afisa Mahusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Emma Nyaki akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Afisa Mahusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Emma Nyaki akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Afisa Usafirishaji kutoka TANESCO Mkoa wa Shinyanga Josephat Anthony akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Afisa Uhusiano TANESO Makao Makuu, Shamu Lameck akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga

Mhandisi wa Mradi wa Umeme Jua Kishapu, Emmanuel Anderson
akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Umeme wa REA III kutoka SUMA JKT Meja James Mhame akizungumza kwenye kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Kikao cha TANESCO na Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments