Ticker

6/recent/ticker-posts

PROFESA NDALICHAKO AANIKA UMUHIMU WA HIFADHI YA JAMII KWA WATANZANIA

 

Na MWANDISHI WETU, ARUSHA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amewataka Watanzania kuona umuhimu wa kujiunga na kuchangia katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Profesa Ndalichako alisema hayo tarehe 22 Novemba, 2023, wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyofunguliwa na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkoani Arusha.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu imeshiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo Kiuchumi’.

Profesa Ndalichako alisema Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine inasimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo kupitia maadhimisho hayo Mifuko hiyo ni sehemu ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kwamba wanapopata fedha wanawajibu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya kesho yao kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

“Ukitembelea mabanda yetu utakutana na Mifuko yote ya Hifadhi yaJjamii ukiwemo wa NSSF ambao unaendelea kuwahamasisha wananchi kuwa na matumizi sahihi ya fedha kwa kujiunga, kuchangia na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye,” alisema Mhe. Profesa Ndalichako.

Post a Comment

0 Comments