Ticker

6/recent/ticker-posts

MWONGOZO WAZINDULIWA TANGA


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MKOA wa Tanga umezindua mwongozo wa uwekezaji ambapo wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo sekta za umma na binafsi zimeshiriki na baadhi yao kueleza mafanikio yao lakini pia kuelezea baadhi ya vikwazo vinavyosababisha kuzorota katika utekelezaji wa majukumu yao

Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona kwa upande wake amesema kihistoria zao la mkonge pekee limeweza kuiingia nchi fedha za kigeni kwa asilimia 65 na hadi sasa nchi ina fursa nyingi za kuwekeza katika kilimo cha zao hilo.



Kambona ameyasema hayo wakati wa kongamano la uwekezaji, biashara na utalii na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Tanga na kueleza kwamba kuna maeneo mengi ya kulima mkonge lakini pia mazao mengine ya mbogamboga na ya chakula.


Amebainisha kwamba katika kuliongezea mnyororo wa thamani zao hilo, mwaka 2019 serikali iliamua kulifanya la kimkakati na kutumia nguvu kubwa sana kuwahamasisha wakulima wa kawaida nao kujikita katika kilimo cha zao hilo.


"Serikali iliona umuhimu mkubwa sana kuchagiza uzalishaji na kuwashirikisha wakulima wadogo ambapo kampeni hii Waziri Mkuu mwenyewe alizindua mwezi machi, mwaka 2020, na mpaka sasa hivi eneo la kilimo kwa wakulima wadogo limeongezeka na kufikia hekta elfu 20 ambalo limeshalimwa" amebainisha.


Naye kutoka Mkurugenzi wa Masoko TPA makao makuu, Dkt. George Fasha amesema bandari ya ni kiungo muhimu cha kuwezesha uhalisi wa jitihada za serikali na wadau kuingia katika uwekezaji halisi katika Mkoa wa Tanga lakini pia ni kiungo kikuu cha uchukuzi katika ukanda huu wa kaskazini mwa Tanzania na nchi jirani.


"Ikiwa na lengo kubwa la kuwawezesha mahitaji muhimu kuingia nchini na kuwafikia wananchi, aidha TPA inatoa shukurani zake za dhati kwa serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji mkubwa iliyoufanya" amesema.


Amefafanua kwamba, "serikali kupitia TPA imefanya mradi mkubwa katika bandari ya Tanga ili kukidhi mahitaji ya wananchi na kufungua fursa za kiuchumi katika upande huu wa kaskazini ambao pia unaiunganisha Tanzania na nchi jirani".


Vilevile Dkt. Fasha amesema serikali imetekeleza miradi miwili ya maboresho katika babdari hiyo ambapo mradi wa kwanza ni kupanua lango la kutokea na kuingilia bandarini, lenye upana wa mita 73, kuongeza kina cha maji kwa kuchimba kutoka mita 3 za awali hadi kufikia mita 13, kupanua eneo la kugeuzia meli kuwa na kipimo cha mita 800 na ununuzi wa mitambo 16 ya kuhudumia sheli.


"Mradi huu wa awamu ya kwanza umegarimu kiasi cha sh bilioni 172.3 ambao umekamilika kwa asilimia 100 na tayari meli kubwa zimeanza kuingia, huku mitambo mipya yenye ufanisi mkubwa ikiwa bandarini, hatua ya sasa ya meli kubwa kutia nanga gatini imeondoa kero ya muda mrefu ya uchukuzi" amesisitiza.


Dkt. Fasha amebainisha kwamba mradi wa awamu ya pili umeiwezesha TPA kufanya maboresho ya gati la zamani kuwa la kisasa likiwa na urefu wa mita 450, kina cha maji 13, yadi ya makasha kontena ya mita za mraba 7230.


"Gati hili lina uwezo wa kuhudumia meli za makasha 2 zenye urefu wa mita 220 pamoja na kubeba hadi tani elfu 60 kwa wakati mmoja, awamu hii ya pili nayo imekamilika kwa asilimia 100 kwa garama ya sh bilioni 256.8,


"Baada ya kukamilika kwa awamu zote mbili za maboresho kwa awamu zote mbili sasa wananchi manufaa yataonekana kwa kila mwananchi kupitia bandari hii" amebainisha Dkt Fasha.

Post a Comment

0 Comments