Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI, MGENI RASMI TAMASHA LA 15 LA JINSIA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UN Women duniani na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Dkt.Phumuzile Mlambo Ngeuka anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la 15 la Jinsia ambalo linatarajiwwa kufanyika Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya TGNP, Mabiboo Jijini Dar es Salaam.

Katika Tamasha hilo takribani watu zaidi ya 2000 wanategemewa kushiriki wakiwemo wawakilishi wa asasi za kirai kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

Vilevile wageni kutoka nchi 14 kutoka mabara matatu duniani watashiriki, nchi hizo ni Ghana, Canada, Korea Kusini, India, Haiti, Eswatini, Afrika Kusini, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe, Bangladesh, Uganda, Kenya na Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Novemba 5,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi TGNP Mtandao, Bi.Gemma Akilimali amesema Tamasha hilo linatambulisha mifumo iliyopo ya uchumi inayounga mkono mapambano ya wanawake na wanaharakati wa ukombozi wa wanawake wanaotaka ugawaji wa haki na usawa wa rasilimali ikiwamo ya maji bajeti za kuhudumia huduma za kijamii, rasilimali asilia kama ardhi, misitu na nafasi za uongozi na upatikanaji wa haki kwa watu wote.

Amesema kuwa tamasha hilo litahusisha mawasilisho, mijadala ya moja kwa moja, maonesho na warsha mbalimbali. Mijadala ya pamoja itajenga dhana halisi kuhusu mada ndogo katika siku husika.

Aidha amesema Maonesho yatafanyika siku zote za Tamasha , yakitoa fursa kwa TGNP, taasisi na mitandao mingine inayoshiriki kubadilishana ujuzi kupitia vyombo vya habari (video, mabango na picha).

"Wachapishaji, azaki na wasanii wa kike wanahimizwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao ambapo jumla ya taasisi na mitandao mingine 42 zimeshajiandikisha kuonyesha kazi zao siku zote za Tamasha". Amesema Bi.Gemma.

Pamoja na hayo amesema kutakuwa na tuzo ya heshima ambapo mama zetu, kinadada, mabinti watakumbukwa kwa mchango wao katika mapambano ya kutetea haki za wanawake, usawa wa kijinsia na haki za kijamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi amesema ndani ya miaka 30 ya TGNP kuna mafanikio makubwa yameibuliwa yakiwemo kuleta chachu ya uchambuzi wa kina wa kijinsia ambapo imeongeza uelewa mpana kwa wanawake, taasisi mbalimbali pamoja na wanaume.

"Kupitia mafunzo ya uchambuzi wa kijinsia yamesaidia kwamba tunapoangalia mifumo kandamizi tuiangalie kwa ujumla wake na si kuangalia moja badala ya lingine. Lakini pia nje ya fanikio hilo tuliweza kuleta sauti na nguvu ya pamoja kupitia majukwaa na mitandao ambapo TGNP ilikuwa ni asasi ya kwanza kuanzisha mitandao ya sauti ya pamoja". Amesema
Mwenyekiti wa Bodi TGNP Mtandao, Bi.Gemma Akilimali akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 5,2023 kuelekea Tamasha la 15 la Jinsia litakalofanyika Novemba 7-10,2023 katika Viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 5,2023 kuelekea Tamasha la 15 la Jinsia litakalofanyika Novemba 7-10,2023 katika Viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 5,2023 kuelekea Tamasha la 15 la Jinsia litakalofanyika Novemba 7-10,2023 katika Viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 5,2023 kuelekea Tamasha la 15 la Jinsia litakalofanyika Novemba 7-10,2023 katika Viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments