Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHAFALI YA 10 CHUO CHA MLVTC YANG'ARA,WAHITIMU WAASWA KUENDELEZA BUNIFU ZAO



**********************

Na Shemsa Mussa,Kagera


Ni katika Mahafali ya 10 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho cha ufundi stadi cha Muleba Lutheran Vocational Training centre kilichopo wilaya ya Muleba Mkoani kagera.
Akizungumza mbele ya wahitimu ,wazazi pamoja na wageni waalikwa Mgeni rasmi katika Mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho,Naibu Katibu Mkuu Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Bukoba katika Kanisa la Kiinjili Kilutheli Tanzania ( KKKT) Bw,Nicolaus Tinkamwesigile,amewaasa wahitimu kujiendeleza na kuendeleza bunifu walizopata chuoni hapo na wasiende kuwa tegemezi kwa wazazi na walezi wao.


"Nawaeleza ukweli hapa jibidiishe sana huko mwendako na sio kukaa kama ndio mmezaliwa leo hamjui lolote ukifanya bidii naamini huwezi kulandalanda mtaani bila kazi,fanya kazi kwa uhaminifu na ujuzi mlioupata hapa MLVTC msikimbilie mjini tafuta fulsa popote nenda mzisaidie hasa zile jamii zinanotumia teknologia bila elimu,amesema Bw Nicolaus"


Aidha ameongeza kuwa ni vema kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na wasiende kuwa vishoka kwa kuharibu miundombinu na taratibu za serikali pamoja na kutaka vitu kwa ulahisi na matokeo yake kujikuta wameshakuwa wezi na kuwa na sifa mbaya katika jamii wanakokwenda,pia amechukua nafasi hiyo amewasihi wazazi na walezi kuwachagulia watoto wao vyuo vyenye maadili na vyenye hofu ya Mungu kwani kufanya hivyo kutaendelea kukemea,kutunza na kudumisha maadili ya Mtanzania.


Nae Mkuu wa chuo hicho cha MLVTC Bw, Benetson Kamugisha amsema chuo cha Muleba Lutheran Vocational Training centre kimeanzishwa rasmi Mwaka 2012 kwa kushirikiana na KKKT/DKMG Jimbo la kusini B pamoja na jimbo rafiki la Paderborn lililopo ujerumani ,pia ameongeza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo katika fani 2 fani ya Tehama (ICT) pamoja na fani ya Umeme (Electrical installation) katika kozi ndefu ya miaka 2 na kozi fupi ya miezi 6.


Pia Bw Kamugisha ameongeza kuwa chuo hicho kilianza kutoa fani hizo 2 kikitambua ni fani zinazotoa mwelekeo wa maisha ukilinganisha maisha ya sasa bila Tehama hayaendi vizuri, pia amesema mbali na darasani wanafunzi hao wamejifunza namna ya kuishi na watu tofauti tofauti kwa kuvumiliana ,kupendana pamoja na kusaidiana katika mambo mbalimbali.


Mkuu huyo wa chuo hicho amesema ni muda wa wazazi na walezi kupokea kijiti kwani wamekaa shuleni ndani ya miaka 2 hivyo wazazi wanatakiwa kuwajengea msingi wanapoenda kuanza maisha mapya mtaani ikiwemo kuwaunganisha na mafundi na wataalamu wenye uzoefu wa fani zao ili kujifunza njia bora ya kutafsiri walichojifunza chuoni.


"Hapa shuleni wamekuwa wakiishi kwa ratiba na sheria za chuo lakini huko mtaani wanapokwenda wanaenda kuishi kwa ratiba zao binafsi watahiyaji kupanga ratba zao wenyewe,nawambia jifunzeni kubadirisha maarifa na ujuzi mlionao kuwa pesa,amesema Bw,Kamugisha"


Kwa niaba ya wahitimu Johanes John na Sakina Ahmada wakati wakisoma risala wameeleza kuwa jumla ya wahitimu ni 17 wasicha 8 wavulana 9 huku wanaochukua fani ya Tehama ni 10 na fani ya Umeme ni 7 huku wakijivunia kupata ujuzi wa mambo mengi ikiwemo kilimo cha migomba , mboga mboga,pamoja na ufugaji wa kuku.


Nao baadhi ya wazazi waliohudhulia Mahafali hayo wameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuwapa elimu na maadili mema watoto wao na kuahidi kutoa ushirikiano kwa pamoja .

Post a Comment

0 Comments