Ticker

6/recent/ticker-posts

KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU 16 GDSS YAKEMEA VITENDO VYA UKATILI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kuelekea Kilele Cha siku 16 za kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Wadau  wa semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) wamekutana  kuwekana sawa juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya Ukatili wa kijinsia nchini ili kuwa na haki na usawa.

Akizungumza kutoka Mabibo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP) Prof.Hassan Salehe Maganga amesema kuwa katika eneo la siasa na utawala ni moja ya sehemu inayochangia kuwepo kwa mfumo dume hivyo kuna haja ya kurekebisha katiba na sheria ya uchaguzi.

Aidha amesema kuwa eneo jingine linalo changia Ukatili ni katika suala la mahari hivyo ameshauri kuwa itungwe sheria ya kupinga mahari  ndoa ijulikane kama mkataba wa watu wawili washirika wa kijamii na kiuchumi.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa Sheria ya ukeketa ni ndogo hivyo ameshauri kuwekwa kwa adhabu ya kifungo cha maisha ili kukomesha kabisa kitendo hicho cha Ukatili kinachoacha madhara ya kudumu na kusababisha kifo .

"Mtu anaye husika awe mlezi awe ngariba wote wakipatikana na sheria wamehusika na ukeketaji wafungwe, wangeogopa kufungwa kifungo cha maisha". Prof.Hassan Amesema.

Kwa upande wake Katibu wa Kituo Cha taarifa na Maarifa Ubungo, Bi.Jamila Kisinga ameeleza kuwa wameadhimia kwenda kutoa elimu kwa jamii kuelekea siku hizo 16 za Ukatili wa kijinsia,kwa kutumia mbinu za kuwafikia makundi ya watu kwenye mikusanyiko nakuwapa elimu.

"Kutoa elimu kwa kutumia mpango wa wana GDSS watatu wanne kuzamia daladala na kupata elimu au kufanya Tamasha big bam na kuwapa elimu ambayo yamezoeleka,au kufanya Bonanza na kukusanya watuna kutoa elimu lakini sisi tuna jamii tunazo ishi tujichukulie Kama jamii tutoe elimu kwenye mikusanyiko ya watu Kama vijiwe vya kahawa na sehemu tofauti tofauti zenye mikusanyiko ya watu"Bi. Jamila Amesema

Naye  Mwanahakati Bi.Agness Lukanga amesema kuwa katika maadhimisho ya siku hizo 16 zinakwenda kuinua mapambano kwa wanawake wajane,walio athirika na virusi vya ukimwi,na walio katika makundi ya ulemav kupambana dhidi ya madhira wanayo pitia.

Siku 16 za Kutokomeza Ukatili wa kijinsia zimezunduliwa Nov 25,2023 na Kilele chake ni Dec 10,2023,zimebeba dhima ya kupinga,kukemea na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa kijinsia ikiwepo pamoja na ubakaji,ndoa za utotoni, ukeketaji,na suala la mfumo dume.

Post a Comment

0 Comments