Taasisi ya Doris Mollel imekabidhi vifaa tiba kwa ajili ya kuanzisha huduma kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es salaam, Vifaa hivyo vyenye thamani ya Milioni 50 vimepokelewa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Ubungo Dkt. Tulitweni Mwinuka ambaye ameishukuru sana Taasisi hiyo na kuwashukuru wasamaria wema waliojitolea kuikumbuka hospitali hiyo haswa katika mwezi huu muhimu wa kuwakumbuka watoto njiti na changamoto zao.
"Vifaa hivi vimetolewa na Msamaria Mwema aliyetamani sadaka yake ifike kwa watoto wanaozaliwa Njiti katika Hospitali hii, baada ya kumuelezea namna ambavyo wanapata changamoto kuwapatia rufaa wakina Mama kwenda katika Hospitali zingine" Doris Mollel
"kwa vifaa hivi tutaanza huduma mapema kabla ya mwaka haujaisha, tutapunguza sana rufaa kwenda Mwanyamala na Muhimbili." Dkt. Tulitweni Mwinuka Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.
Kwa Upande wake Daktari wa Watoto Dkt. Edith Shirima amebainisha kuwa huwa wanawapa rufaa watoto 10 mpaka 16 kwa mwezi kwenda Hospitali ya Mwananyamala au Muhimbili kwa ajili ya huduma hiyo.
0 Comments