SEKTA ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo ya Taifa 2011/12 hadi 2024/25, inatarajiwa kuleta maendeleo ya rasilimaliwatu kwa kutayarisha Watanzania mahiri walioelimika na wapendao daima kujielimisha ili kuliletea Taifa maendeleo na kuliweka kwenye uchumi shindani.
Ili kufikia lengo hilo, mfumo wa elimu na mafunzo unaotumika nchini lazima utoe fursa za kutosha kwa watu wengi zaidi kuelimika na kuendelea kujielimisha. Kadhalika, mfumo huu unawajibika kutoa elimu na mafunzo yenye ubora unaokubalika na kutambulika kitaifa, kikanda na kimataifa.
Elimu ina maana pana sana ila ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi., elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.
Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo ,kama vile kuandika, kusoma, kuhesabu (hisabati), sayansi na historia.
Mwaka 2015 chini ya Rais Hayati John Pombe Magufuli, Serikali ya Jamhuli ya Muungano wa Tanzania iliweka sera juu elimu bure,yaani (Elimu bila Malipo) kuanzia awali mpaka kidato cha nne ,na kupitiwa na kutekelezwa katika mwaka wa masomo 2016/17, ambapo serikali ilisema itahakikisha elimu ya awali mpaka kidato cha nne inakuwa ya bure na lazima katika shule zote za umma.
Neno [Elimu bure,bila Malipo ] limepoteza maana kwa kuathiriwa na Michango Michango Mingi inayoendelea kufanyika kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari katika wilaya mbalimbali za mkoa wa kagera.
Richa ya kuwepo changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa sera hiyo ,bado serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia na kutekeleza sera hiyo kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwamo kujenga Vyumba vya madarasa,pamoja na kutoa ghalama na kiasi kadhaa kwa ajili ya uendeshaji wa masoma kila Mwezi.
Kwa Mtazamo huo sikusita kutaka kujua hali ikoje kwa sasa na nimebahatika kukutana na baadhi ya wanafunzi kutoka shule tofauti ndani ya Mkoa Kagera wakiwemo Jasinta Jastine,Nerson Dominick , Elivira Abdon na Sharifu Shafi na kueleza kuwa suala la elimu bila Malipo ni jambo jema ila limefanya wazazi wengi kubweteka na kusahau majukumu yao kama wazazi.
"Kuna baadhi ya mahitaji ya shule tumekuwa tukitumwa na waalimu nyumbani, ila muda mwingine kama mzazi hana inabidi ukae nyumbani hadi ulichotumwa kikipatikana ndio utarudi shule hilo ni tatizo kwetu maana tunaowaacha shuleni wanaendelea na masomo hawatusubiri,mpaka chakula mfano shuleni kwetu sisi kuna uji tu ila wazazi wetu wamekuwa wagumu sana kuchangia wakati tunakunywa sisi wenyewe tunachokishauri sisi, wazazi wameshapunguziwa mzigo wa kulipia ada basi mambo mengine ni ushirikiano tu na hapa mfano kama mimi Jasinta nakaribia kujitimu wazazi wengi wanahangaika na michango ya sherehe ambayo mimi kwa upande wangu sioni kama ni faida na muhimu kama kupata chakula shuleni ,wameeleza wanafunzi hao "
Sikusita kuwatafuta wazazi na kutaka kujua wanaielewa vipi elimu bure na ni wakati gani wanaupitia katika kutoa mahitaji yanayotakiwa shuleni na je wana haki ya kusaidizana na serikali kwenye hilo? Nae Bi Husna Hussen na phajence Nerico wamesema ni wajibu wa kila mzazi anajua na kufuatilia haki za mtoto ikiwemo elimu na kutoa ushirikiano pale anapotekea wa kumshika mkono katika suala hilo na kuwashauli waalimu kuhitisha mikutano pindi panapohitajika kitu cha kuchangia na sio kuandika barua na kuwarudisha watoto nyumbani kwa ajili ya suala hilo.
"Mtoto anaenda shule asubuhi ila muda si kidogo unamuona tena amerudi ukimuuliza anakwambia tumetumwa hela ya mlinzi au hela ya mtihani au chochote kinachohitajika muda mwingine hata sisi wenyewe bila kujua kwa wakati huo mimi nafanya nini nyumbani au nina hali gani na unasikia mtoto anasema nimeambiwa nisipofanya nilichoambiwa nisirudi, mikutano ya shule ni muhimu inaweka utaratibu wa kutujuza na kutupatia muda wa kujipanga,Mtoto ni wa kwangu kutoa ushirikiano ni sahihi ila walimu waweke utaratibu mzuri sio kukimbizana kimbizana, wemesema wazazi hao"
Walimu nao sikuwaacha nyuma kuuelezea umma namna wao wanavyotekeleza sera na maagizo ya serikali na ni vipi wazazi wanatoa ushirikiano kwenye hilo na wamejipanga vipi kuweka utaratibu ulio mzuri na hapa Mwalimu Aidath Saad ambaye pia ni Mkufunzi katika fani ya ICT amesema kuna changamoto za kiuelewa kwa baadhi ya wazazi wakizani wakichangia chakula kwa watoto wao sisi walimu tunabeba na kupeleka majumbani kwetu kitendo ambacho hakiwezekani na muda mwingine baadhi ya wazazi huwapatia pesa nyingi watoto wao ya kutumia njiani kununua vitu ,vyakula) ila 500 ya uji inakuwa ngumu kuitoa ,badhi pia ni wabinafsi huku wakifikilia kuchangia wanadhani wanawachangia wengine muda mwingine tunatoa mufukoni kwetu ili kukamilisha zoezi la kifu fulani.
"Jamani serikali ya Mama Samia inafanya mambo mengi pamoja na kuwalipia ada watoto wenu na uji au chakula mnataka mlipiwe kweli,wazazi litambueni hilo jambo ,huyo mtoto akishafahulu na kuajiliwa wanufaika wakubwa ni nyie wazazi ,nasema mtoto ni wenu nikimaanisha mfano ukiwa unaozesha anayepokea mahali ni wewe na sio serikali hivyo ushirikiano ni muhimu na kupendana pia kama mtoto anaona hautoi hata senti ama hauhangaiki kwa ajili yake ataona elimu ni mchezo tu wala hawezi kuweka bidii, kuweni na uchungu na haki za watoto wenu amesema Mwalimu Aidath"
Nao Maafisa waliyopewa mamlaka ya kuisimamia elimu ndani ya Manispaa ya Bukoba Bw. Baseki Sheja Afisa Elimu Awali na Msingi na Bw Francis Nshaija Afisa Elimu Sekondari wameukumbusha umma nini maana ya elimu bure na kupata nafasi ya kuwaeleza wananchi nia na dhamila ya serikali katika suala hilo la elimu bure na kueleza wajibu wa wazazi kwenye hilo na kusema serikali iliweka utaratibu huo kwa lengo kwa kuwasaidia wazazi na kutoa kurikiano katika sekta ya elimu na kusema kuwa kwa hatua hizo serikali imetoa fedha kwa ajili kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Wameongeza kuwa katika taratibu za kuchangia suala la elimu ni jukumu la wazazi wao kwa wao bila kushirikisha walimu na kwa kufuata sheria ikiwemo kupata kibari cha nini wanataka kuchangia na wapi.
Aidha wameeleza kuwa lazma kuwepo mkutano kwa ajili ya kukutana na kukubalia kwa jambo furani na sio kutumia nguvu na mgambo kwenye hilo na kusema kuwa jukumu la mwalimu ni kushawishi wazazi na walezi kuona wanalolichangia lina umuhimu gani kwa watoto wao na kwenye jamii kwa ujumla huku serikali na wadau wengine wakiendelea kuziba mianya ya mahitaji katika sekta hiyo.
Pamoja na sera hii kuleta faida kubwa kwa wazazi lakini imepeleka mzigo mkubwa kwa wakuu wa shule pamoja na wenyeviti wa kamati za shule ,Wazazi wengi wanadhani jukumu la kupata elimu kwa watoto wao ni la serikali peke yake.na kusahau suala la kupata elimu iliyobora ni jukumu na ushirikiano wa pamoja kati ya serikali, wazazi/walezi na wanafunzi.
Jambo la msingi ni kwamba michango isiwe ya lazima lakini kama wakuu wa shule na kamati za shule wanaweza kutumia utashi wao na kuwashawishi wazazi na wadau wa elimu kushirikiana kwa umoja.Hii itawezesha wakuu wa shule,wazazi, walimu na kamati za shule kupunguza changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini Tanzania, na itasaidia kuboresha elimu kwa ujumla.
Kwa mantiki hiyo elimu bila malipo italeta unafuu kwa wote nakutoa manung'uniko kwa baadhi ya watu shule nyingi za serikali zinakumbwa na changamoto nyingi hivyo ni wajibu wa kila mzazi kushirikiana na serikali ,ewe mzazi /mlezi ukiwa unajiuliza elimu bila malipo au elimu bure ni nini tafakhari pia mtoto au mwanafunzi ni wa nani na ni elimu bila malipo sio elimu bure
0 Comments