Ticker

6/recent/ticker-posts

BOB JUNIOR AOMBWA KUPEWA MCHONGO VANILLA INTERNATIONAL

  

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Limited Simon Mnkondya

***
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Limited Simon Mnkondya amemkaribisha Msanii Bob Junior kuwekeza kwenye Kilimo cha Vanilla ili kukuza soko la zao hilo ambalo linazidi kupata umaarufu kila kukicha kutokana na kuwa na thamani kubwa duniani.

 Mkondya amesema Kampuni ya Vanilla International Limited  ina mashamba makubwa ya kilimo cha vanilla duniani kwa njia ya Greenhouses ikiwa na mradi mkubwa kuliko yote ya kilimo cha vanilla duniani na wanafanya kilimo hicho kwa njia za kisasa wakiwa wamekuchukua Teknolojia Israel.

"Ninamkaribisha sana ndugu yangu Bob Junior ambaye amehitimu Elimu yake katika nchi iliyoendelea ya Finland katika degree ya TELECOMMUNICATION,  ameonekana kuwa atakuwa mtu muhimu sana katika kufanya kazi na Kampuni ya Vanilla International Limited kwani kwa level aliyoifikia ni kubwa na anau wezo wa kukuza soko la vanilla hasa katika nchi za Ulaya hususani Finland ambayo ni watumiaji wakubwa wa vanilla na bidhaa zake",amesema Mnkondya.

Mnkondya amesema Vanilla International  Ltd iko tayari kumlipa mshahara mkubwa  Msanii Bob Junior kwani ataipeleka kampuni mbali endapo atakubali kufanya kazi na kampuni ya VANILLA INTERNATIONAL LIMITED.

Amesema licha ya kumhitaji Msanii Bob Junior pia wanawakaribisha wasanii wote ambao wameyumba kimziki na kisanii kwa namna moja au nyingine kama Sister P, DuduBaya, Domo Kaya, Juma Nature, Mr.Nice, Zay B, Nyamayao, Mhogo Mchungu, Kibakuli, Rich Mavoko, Matonya na wengine wengi waje Vanilla Village Dodoma ili wapromote na kukuza kilimo cha Vanilla Nchini.

Wasiliana na Kampuni ya Vanilla International Limited  kwa simu namba 0629300200

Post a Comment

0 Comments