Wapenzi wa mpira wa miguu nchini Tanzania wana nafasi ya kushinda tiketi kwenda Ivory Coast kushuhudia timu ya taifa ya soka ya wanaume ‘Taifa Stars’ ikichuana kuwania Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON). Kupitia promosheni ya Twende AFCON inayoendeshwa na kampuni ya Betway Tanzania, mashabiki wanne wana nafasi ya kushinda tiketi kwenda Ivory Coast kuiunga mkono Taifa Stars iliyofuzu mashindano hayo.
Taifa Stars wameandika historia kwa kufuzu michuano ya AFCON kwa mara ya tatu pekee tangu kuanza kwa mashindano hayo yenye hadhi ya juu zaidi katika soka barani Africa. Betway Tanzania imezindua rasmi promosheni hiyo ya mwezi mmoja iliyoanza rasmi Novemba 16 na kuendelea hadi Disemba 16, 2023 kwa lengo la kuiongezea hamasa timu ya Taifa Stars pamoja na kuwapa wateja wake na mashabiki wa mchezo wa soka kwa ujumla nafasi ya kuwa sehemu ya historia ya soka la Tanzania.
Ili kushiriki katika promosheni hii, mshiriki anapaswa kujisajili na kubashiri mchezo wowote na Betway kwa kiwango cha kuanzia shilingi 100 kupitia mtandao wowote wa simu katika kipindi kati ya Novemba 16 na Disemba 16, 2023. Kila ubashiri utaingiza kwenye droo ya bahati, ambapo mshindi atajishindia tiketi kwenda Ivory Coast.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo iliyofanyika ofisi za Betway jijini Dar es Salaam, Jimmy Masaoe, Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, amesema;
"Tunafurahi kuwa sehemu ya historia ya mpira wa miguu nchini Tanzania kwa kuhakikisha Watanzania wanaiunga mkono timu ya taifa katika mashindano makubwa zaidi ya mpira barani Africa. Promosheni hii ni moja ya njia ya sisi kuisadia timu yetu ya taifa na kutoa fursa kwa mashabiki kushuhudia mashujaa wa nchi wakipeperusha bendera huko Ivory Coast.”
Kwa upande wake Calvin Mhina, Meneja Masoko wa Betway Tanzania, pia aliwahimiza mashabiki wa michezo na wateja wa Betway kushiriki katika promosheni na kuitumia kama fursa ya kuiunga mkono timu ya taifa huku wakibashiri kistaarabu.
"Hii ni fursa ya kipee na nzuri kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini Tanzania. Usikose nafasi hii ya kushinda tiketi kwenda AFCON na kushangilia Taifa Stars. Jisajili na Betway leo na weka ubashiri wako kuingia kwenye droo. Unaweza kuwa mmoja wa washindi wenye bahati kusafiri kwenda Ivory Coast na kuwa sehemu ya historia mpya katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla."
“Kila shabiki anaweza kubashiri michezo anayoitaka na kuanzia kiwango cha chini kabisa cha shilingi mia moja. Tumefanya hivi ili kuhakikisha washiriki wanabashiri kistaarabu kama ambavyo kauli mbiu yetu imekuwa ikisisitiza.” Aliongeza Mhina.
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2024 ambalo itafanyika nchini Ivory Coast limepangwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024. Mashindano yatajumuisha timu 24 zikiwania kombe hilo lenye thamani zaidi barani Africa. Tanzania, baada ya kufuzu kwa mara ya tatu tu tangu ilipofuzu mwaka 1980 na 2019 tangu kuanzishwa kwa AFCON, itaanza kampeni yake katika Kundi F dhidi ya Morocco Januari 17, ikifuatiwa na mechi dhidi ya Zambia Januari 21, na DR Congo Januari 24.
0 Comments