Mkuu wa Uendeshaji NBC Bi. Alelio Lowassa (aliesimama) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tambaza iliyopo Manispaa Ilala jijini Dar es Salaam walioshiriki semina fupi ya mafunzo kuhusu elimu ya fedha na akiba iliyoendeshwa na benki hiyo shuleni hapo jana. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Hussein Mavumba (wa pili kulia), walimu na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza iliyopo Manispaa Ilala jijini Dar es Salaam Mwalimu Hussein Mavumba (aliesimama) akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo walioshiriki semina fupi ya mafunzo kuhusu elimu ya fedha na akiba iliyoendeshwa na benki ya NBC shuleni hapo jana. Wanaomsikiliza ni pamoja na maofisa waandamizi wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC,Bi Salama Mussa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi wa Mahesabu wa benki hiyo Bw Fulgence Shiraji (wa tatu kushoto)
Mkuu wa Uendeshaji NBC Bi. Alelio Lowassa (kushoto) akikabidhi mpira wa miguu kwa Mwalimu Nicholaus Nolasco ambae ni mwalimu wa Michezo Shule ya Sekondari Tambaza ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya zawadi zilizotolewa na benki hiyo kwa uongozi na wanafunzi wa shule hiyo wakati semina fupi ya mafunzo kuhusu elimu ya fedha na akiba iliyoendeshwa na benki hiyo shuleni hapo jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Hussein Mavumba (wa pili kshoto), walimu, wanafunzi na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi wa Mahesabu wa benki ya NBC Bw Fulgence Shiraji (kushoto) akikabidhi mpira wa miguu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tambaza ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya zawadi zilizotolewa na benki hiyo kwa uongozi na wanafunzi wa shule hiyo wakati semina fupi ya mafunzo kuhusu elimu ya fedha na akiba iliyoendeshwa na benki ya NBC shuleni hapo jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Uendeshaji NBC Bi. Alelio Lowassa (katikati) na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Hussein Mavumba (wa pili kulia)
Mafunzo hayo yalihusisha uwasilishwaji wa mada mbalimbali kuhusu masuala ya fedha, ujasiriamali pamoja na kutoa fursa kwa wanafunzi hao kujibu na kujadili hoja mbalimbali kuhusu mada hizo.
Meneja Huduma wa Benki ya NBC Bw. Stanley Munisi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tambaza iliyopo Manispaa Ilala jijini Dar es Salaam walioshiriki semina fupi ya mafunzo kuhusu elimu ya fedha na akiba iliyoendeshwa na benki hiyo shuleni hapo jana.
NBC Daima! Baada ya semina hiyo viongozi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji NBC Bi. Alelio Lowassa (wa tano kushoto) ulipata wasaa wa kupiga picha ya pamoja na walimu walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tambaza wakiongozwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Hussein Mavumba (katikati).
Mkuu wa Uendeshaji NBC Bi. Alelio Lowassa (Katikati) sambamba na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi wa Mahesabu wa benki hiyo Bw Fulgence Shiraji (kushoto) na Mkuu wa shule ya Sekondari Tambaza Mwalimu Hussein Mavumba (kulia) wakipanda moja ya mti wa matunda kwenye viunga vya shule hiyo ikiwa ni kumbukumbu ya ziara ya maofisa hao shuleni hapo kwa ajili ya semina fupi ya mafunzo kuhusu elimu ya fedha na akiba kwa wanafunzi. Wanaoshuhudia ni maofisa wengine wa benki hiyo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC wakipanda moja ya mti wa matunda kwenye viunga vya shule ya Sekondari Tambaza ikiwa ni kumbukumbu ya ziara ya maofisa hao shuleni hapo kwa ajili ya semina fupi ya mafunzo kuhusu elimu ya fedha na akiba kwa wanafunzi. Wanaoshuhudia ni maofisa wengine wa benki hiyo.
0 Comments