[Dar es Salaam; Novemba 6, 2023] Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana ilinogesha shangwe za mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kwa kuwapeleka uwanjani wateja wake pamoja na wadau mbali mbalimbali wa benki hiyo ili kushuhudia mtanange huo ulioisha kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba.
Aidha benki hiyo pia iliandaa matukio mbalimbali kwa ajili ya mashabiki wa soka pamoja na wateja wake katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam na Mwanza huku pia ikitumia mechi hiyo kubwa kuzindua rasmi kampeni maalum ya msimu wa huu wa soka inayofahamika kama ‘Soka Limeitika’ ambayo inalenga kuhamasisha na kujivunia mafanikio ya mchezo huo kutokana na udhamini wake kwenye ligi hiyo.
Katika tukio kubwa lililofanyika hotel ya Hyatt Regency Dar es Salaam, ilishuhudiwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi akiongoza hafla fupi ya chakula cha mchana maalum kwa ajili ya baadhi ya wateja wakubwa na wadau wengine wa benki hiyo, tukio lililofuatiwa na msafara maalum kuelekeaUwanja wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo.
“Tumetumia mechi hii kubwa ili kwa pamoja tuweze kujumuika na kufurahia sambamba na wadau wetu hawa muhimu. Lengo ni kupata wasaa mzuri ili kufurahia pamoja ile ladha ya mchezo huu pendwa. Wote kwa pamoja tutakwenda uwanjani katika msafara maalum na baada ya mechi tutarudi pamoja kutoka uwanjani hadi hapa hotelini kisha tutaachana huku kila mmoja akienda kwake akiwa salama kabisa,’’ alibainisha Sabi.
Akizungumzia kwa kina kuhusu kampeni ya ‘Soka Limeitika’ Meneja Masoko wa benki ya NBC Bi Alina Kimaryo alisema mbali na kuhamasisha ari ya mchezo huo pendwa, kampeni hiyo inalenga kujivunia mafanikio ya mchezo huo yaliyopatikana kutokana na udhamini wa benki ya NBC kwenye ligi hiyo inayozidi kujiongezea umaarufu barani Afrika na ulimwengu kwa ujumla.
“Tangu tuwekeze nguvu kwenye ligi hii benki ya NBC na wadau wa mchezo wa soka tumeshuhudia mafanikio mengi ya kujivunia ikiwemo kuongezeka kwa ubora wa ligi yetu kitaifa na kimataifa ambapo nafasi ya ubora wa ligi yetu kwa viwango vya bara la Afrika kwasasa ni nafasi ya 5 kutoka nafasi 12 tuliyoikuta wakati tunaanza udhamini wetu. Pia udhamini wetu umeviongezea uwezo wa kiuchumi vilabu vinavyoshiriki ligi hii na sasa vipo imara kwenye eneo hilo na ndio sababu sasa hata mechi zinafanyika kulingana na ratiba bila vilabu kukwama kufika viwanjani kutokana na ukata,’’ alibainisha.
Aidha alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na utoaji wa Bima za afya kwa wachezaji, familia zao na bechi la ufundi, mikopo ya mabasi inayolendelea kutolewa na benki hiyo kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi hiyo, ubora wa viwanja, udhamini wa benki hiyo kwenye ligi ya NBC Championship na ligi ya Vijana (Youth League) sambamba na uboreshaji wa huduma ya mauzo ya tiketi za michezo ya ligi hiyo kupitia mawakala wa benki hiyo waliopo maeneo mbalimbali nchini.
“Ni wazi kwamba udhamini wa NBC umeongeza vipato kwa vilabu ndio sababu sasa tunashuhudia vilabu vinaweza kusajili kwa ushindani wachezaji bora kutoka ndani na nje ya nchi hatua ambayo inaviwezesha kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa. Hamasa hii inayoshuhudiwa sasa kwenye mchezo huu pia ni matunda ya udhamini wa NBC na hiyo ndio maana halisi ya ‘Soka limeitika,’ alimalizia Alina.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wateja pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa na wadau hao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga iliyoisha kwa kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba.
Mkurugenzi Mtendaji Benki ya NBC, Theobald Sabi (Kushoto) akibadilishana mawazo na wateja pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa na wadau hao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga iliyoisha kwa kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (Kulia) akibadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa na wadau hao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga iliyoisha kwa kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Brendansia Kileo akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wateja pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa na wadau hao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga iliyoisha kwa kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wateja pamoja na wadau mbalimbali wa benki ya NBC waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa na wadau hao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga iliyoisha kwa kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba.
0 Comments