Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amekutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya Christine Grau jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana kuhusu ushirikiano wa kikazi katika Sekta ya madini hususani katika kuendeleza na kuibua fursa mpya zilizopo ndani Sekta ya madini kwa kufanya tafiti mbalimbali ili kuwa na taarifa za nchi nzima.
Mhe. Mavunde alimweleza Balozi Grau kuhusu mikakati ya Serikali kupitia VISION 2030 kuwa mpaka sasa uwekezaji katika ya Madini umetumia taarifa za utafiti jiofizikia zilizofanywa kwa asilimia 16 tu hivyo ifikapo mwak 2030 Serikali imepanga kuwa na kanzidata yenye taarifa za utafiti wa Jiofizikia kwa asilimia Mia moja.
0 Comments