Ticker

6/recent/ticker-posts

Wavuvi Kagera watakiwa kufanya shughuli zao kwa kuzingatia usalama na kuepuka kuingia majini wakiwa wamelewa .


***************

Na Shemsa Mussa, Kagera.

Agizo hilo limetolewa na katibu tawala msaidizi mipango na uratibu Nestori Bwana kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa huo ,Toba Nguvila wakati akifungua kikao cha kutambulisha mradi wa kuzuia ajali za majini ,ambao unaratibiwa na shirika la Emedo kilichofanyika katika manispaa ya Bukoba kwa kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo jeshi la zimamoto na uokoaji pamoja na jeshi marine.

Amesema kuwa wavuvi hao wanatakiwa kutambua kuwa uhai wao ni muhimu kuliko uvuvi wanaoufanya bila kufuata sheria , hivyo wahakikishe wanachukua tafadhali zote zinazotakiwa kipindi wanapoenda ziwani kwa shughuli zao za uvuvi Ili kujikinga na ajali zisizokuwa za lazima na ambazo zimekuwa zikipoteza uhai wao.

Kwa upande wake meneja mradi kutoka shirika la Emedo bwana Arthur Mugema amesema kuwa kutokana na utafiti waliofanya kwenye baadhi ya mialo katika ziwa victoria ikiwemo mwalo wa kisiwa cha Kerebe wamebaini kuwa ajali nyingi zinazotokea zinatokana na uzembe unaofanywa na waajili na wavuvi kwa kutokuchukua taadhali zinazotakiwa pamoja na baadhi ya wavuvi kwenda ziwani wakiwa wamelewa.

Hata hivyo ameongeza kuwa sababu nyingine waliyoibani ni kutokana na mitumbwi Mingi kutumia mbao ambazo hazikidhi viwango na huku baadhi ya mitumbwi kuwekwa viraka vya mabati kwani kwa mkoa wa Kagera zaidi ya mitumbwi elfu moja imeeekwa viraka

Post a Comment

0 Comments