Ticker

6/recent/ticker-posts

WAHITIMU UDSM WAHIMIZWA KUTUMIA MAARIFA NA UJUZI WAO KULETA MABADILIKO KWENYE JAMII

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wametakiwa kuwa wazalendo kwa kutumia maarifa na ujuzi waliopata wakiwa shule kwa kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii zao hasa katika kuleta maendeleo.

Wito huo umetolewa leo Oktoba 17,2023 na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye wakati wa Mahafali ya Hamsini na Tatu (53) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

Amesema kuwa elimu haiwezi kuleta faida na kuwa chachu ya mabadiliko yaliyokusudiwa kama haitatumiwa katika kutatua matatizo ya jamii.

“Endapo ajira Serikalini au katika sekta binafsi zitachelewa kupatikana kuweni wepesi kuangalia sehemu nyingine ambapo maarifa na ujuzi wenu unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi”. Amesema

Pamoja na hayo ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa rasilimali muhimu zinazohitajika katika uendeshaji wa Chuo.

“Serikali imeendelea kugharamia na kudhamini mafunzo ya wafanyakazi wa kada mbalimbali na kuwapa stahiki zao muhimu za kiutumishi”. Amesema Prof. Anangisye.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Mwanaidi Maajar amesema kuwa Baraza linaendelea kusimamia kwa weledi miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa (HEET) ambapo liliidhinisha uanzishwaji wa kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mkoa wa Kagera na Lindibna mradi unahusisha ujenzi wa Kampasi hizo, pia ukarabati wa baadhi ya majengo katika Kampasi zilizopo Mwalimu Nyerere Mlimani, CoICT Kijitonyama, SoAF Kunduchi na IMS, Buyu-Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete akiwatunuku Shahada za awali, Stashahada na Astashahada Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya 53 (Duru ya Pili) ya Chuo hicho leo Oktoba 17,2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa amesimama kuimba wimbo wa Taifa katika Mahafali ya 53 (Duru ya Pili) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Oktoba 17,2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akisoma hotuba yake katika katika Mahafali ya 53 (Duru ya Pili) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam leo Oktoba 17,2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakiwa kwenye Mahafali ya 53 (Duru ya Pili) ya Chuo hicho leo Oktoba 17,2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments