Na Shemsa Mussa,Kagera.
Mamlaka ya Mapatao Tanzania (TRA )Mkoa wa Kagera imetoa Elimu kwa Waandishi wa habari wa Mkoa huo iliyolenga kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya ulipaji kodi ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mazuri kati ya mamlaka hiyo na Wanahabari.
Akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa E.L.C.T uliopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Afisa Elimu na Mawasiliano TRA Mkoa wa Kagera Rwekaza Rwegoshora alisema pasipo kulipa na kukusanya Kodi hakutakuwa na maendeleo na kuwa inapotokea mlipa kodi akachelewa kulipa kodi kwa wakati pia uchelewesha maendeleo ambayo humsaidia kupata huduma muhimu.
Rwegoshora aliongeza kuwa ni wajibu wa mlipa kodi na mfanyabiashara yoyote kutunza kumbukumbu za biashara yake kwani asipotunza kumbukumbu hizo anapokadiliwa kodi inaweza tokea akakadiliwa kikubwa au kidogo kutokana na kutotunza kumbukumbu.
Aidha amesema ni muhimu kwa anayeuza kutoa risiti kwani bila kufanya hivyo faini yake ilishapitishwa kuanzia Julai mosi mwaka 2023 ambapo atalipa kikubwa Kati ya sh Milioni 1 na laki 5 au asilimia 20 ya bidhaa au huduma alisema mnunuaji anapobainika amefanya manunuzi bila kudai risiti faini ni sh 20,000 au asilimia 20 ya kodi iliyokuwepo hivyo nawakumbusha faini sio nzuri kwa biashara zetu hivyo daini risiti na toeni risiti.
Pia alisema kuwa anaamini semina hiyo itakuwa chachu kwa Wanahabari kutoa Elimu hiyo kupitia vyombo vyao kwa jamii huku akitoa wito kwa Wafanyabishara na Wananchi kutambua kuwa kodi ndiyo maendeleo hivyo walipe kwa wakati ili kuruhusu maendeleo kuwepo kwa haraka.
Kwa upande wake Afisa Elimu na Mawasiliano Isihaka Shariff kutoka Dar es salaam alisema kuwa Wafanyabishara wataendelea kupata haki yao ikiwa ni pamoja na elimu ya Kodi, kuhudumiwa bila upendeleo ambapo pia aliwasisitiza kuendelea kutunza kumbukumbu za biashara zao ili kuepuka hasara.
Hata hiyo naye Afisa Msimamizi Mkuu wa wa elimu na Mawasiliano Bi Lydia Shio aliwapongeza Wanahabari kwa mafunzo hayo na kuwaomba Wafanyabishara kuona umuhimu wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Nchi na kuwaomba Watanzania kutoa taarifa inapotokea wamebaini wanaokwepa kulipa kodi au watumishi wa TRA wanaokiuka maadili.
0 Comments