Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS KANDA YA MASHARIKI YATEKETEZA VIPODOZI TANI NANE VYENYE VIAMBATA SUMU

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Mashariki limeteketeza tani nane ya bidhaa za vipodozi vyenye viambata sumu ambazo zilikamatwa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Jana Oktoba 6,2023 Mkuranga mkoani Pwani, Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Bw.Francis Mapunda amesema zoezi la kukamata bidhaa za vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku ni endelevu hivyo amewataka wafanyabiashara kuacha kuuza bidhaa hizo.

Aidha alitoa wito kwa wafanyabiashara wa vipodozi kufanya usajili wa vipodozi na kufuata orodha ya bidhaa za vipodozi ambavyo vimesajiliwa na kuruhusiwa kuuzwa.

Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanajiepusha na biashara ya bidhaa za vipodozi zenye viambata sumu vilivyopigwa marufuku kuepusha usumbufu na gharama zisizo za lazima.


Post a Comment

0 Comments