Na Shemsa Mussa ,Kagera .
Taasisi ya kilimo na utafiti tanzania ( Tanzania Agricultural Research Insutitute,(TARI) kanda ya ziwa imefanya kikao leo kwa lengo la kujadili na kutathimini shughuli za kilimo na utafiti ndani ya mwaka mzima, kikao hicho kimefanyika katika kumbi za ELCT Manispaa ya Bukoba kimekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo pamoja na wageni kutoka katika vituo vingine vya utafiti huku walengwa wakuu wakiwa ni kituo cha utafiti Maruku na kutuo cha Ukiriguru Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa kituo cha utafiti Maruku Dkt Mpoki Shimwela ,amesema kuwa kila mwaka hukutana kwa lengo la kujadili shughuli zilizofanyika ndani ya mwaka mzma na kujua ni wapi panatakiwa kuboreshwa zaidi na nini kifanyiwe utafiti pamoja na kupeana mipango kazi ya mwaka unaokuja na amesema kuwa kwa upande wa kituo cha Maruku wanajihusisha na utafiti wa mazao mbalimbali hasa Migomba (Ndizi),Viazi ,Mihogo pamoja na Kahawa kwa usimamizi wa Tanzania Coffee Research Institute (TACRI)
Aidha Dkt Mpoki ameongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha serikali imetenga kiasi cha shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara ya kuzalisha Mbegu mbalimbali hasa Migomba na kahawa na kusema ujenzi huo utamsaidia mkulima kuondokana na ghalama kubwa ya nunuzi wa mbegu ikiwa sasa mkulima ananunua mbegu kuanzia kiasi cha shilingi 2500 hadi 3000 na endapo Maabara hiyo ikikamilika mkulima ataweza kununua mbegu kwa shilingi 500 hadi 1000 na pengine kugawiwa bure .
"Kama mnavyojua siku si nyingne mhe waziri Hussein Bashe alisema kuhusu Kujengwa kwa maabara hapa kagera na jengo hilo litajengwa Maruku wananchi watanufaika pakubwa sana nitoe shukuran kwa Rais samia kwa kile anachokifanya katika sekta ya kilimo na pongezi kwa waziri wetu Bashe kwa kuendelea kuisemea sekta ya kilimo,amesema Dkt Mpoki "
Nae Dkt Paul Saidia Meneja wa kituo cha utafiti Ukiriguru ambaye pia ni mtaalamu wa zao la pamba amesema zao hilo limekuwa likisumbuliwa na wadudu pamoja ukosefu wa udongo wenye rutuba na hivyo kupelekea zao hilo kushuka katika uzalishaji na kwasasa wameanza zoezi la kutoa elimu na kuwapatia wakulima mbegu za pamba ili kuongeza uzalishaji ,na katika kilimo cha Mihogo wanazo mbegu 6 bora na aina ya (Tarikasifour) imeonekana kupendwa zaidi huku viazi lishe zikiwa mbegu 9 zenye vurutubisho mbalimbali.
Kwa upande wake Dkt Furaha Fremon Mroso Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya utafiti na ubunifu TARI Makao Makuu amesema jukumu la Tari ni kufanya tafiti zote za kilimo na kuhakikisha tafiti hizo zinawafikia wahusika ambao ni wakulima pamoja na kuratibu shughuli zote za kilimo,ameongeza kuwa mpaka sasa Tari inavyo jumla ya vituo vya utafiti 17 ndani ya Tanzania hivyo ni lazma kila kituo kujua utekelezaji wa kazi yake na kujua nini kinafanya.
"Kama huwezi kujua ulipo naamini huwezi kupanga yajayo hivyo lazima tukae vikao kama hivi ili kujua tulipo na kuanga nini tufanye niwapongeze sana kwa kuja amesema Dkt Furaha "
Aidha kwa upande wake Bw Louis Baraka Afisa kilimo Mkoa kagera aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho ameipongeza Tari kwa tafiti inazoendelea kufanya na kuwasisitiza wakulima kuzingatia kile wachoelezwa kutoka kwa wataalamu wa kilimo ikiwemo kuendana na mabadiliko ya tabia nchi na utumiaji sahihi wa mbegu bora pamoja na mbolea ili kuongeza kasi na kiwango cha uzalishaji wa mavuno .
0 Comments