SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu imebainisha kuwa itaendelea kushirikiana na nchi ya Norway kwa kuunganisha watafiti wa nchi hizo ili kubadilishana uzoefu na hivyo kuwezesha ufanyikaji wa tafiti zenye ufanisi na tija katika mendeleo ya taifa.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ambapo amesema kuwa kwa sasa nchi hizo zinatekeleza Miradi 18 ndani ya vyuo 9 tofauti nchini lengo likiwa ni kujaidil na kuona namna bora ya kuendelea na tafiti hizo
Kwa upande wake Kaimu Naibu Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam anayeshughulika na masuala ya Utafiti prof. Nelson Boniface amesema baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi hiyo kuwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya kufundishia na kufanya tafiti sambamba na kutoa wataalamu wenye umahiri katika ufanyaji wa tafiti
Naye Balozi wa Norway nchini Tanzania amesema kuwa lengo ni kujifunza zaidi juu ya ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili na kusisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na wataalamu mbalimbali kutoka nchini ili kuwezesha ufanyikaji wa tafiti zenye tija katika maendeleo ya jamii.
0 Comments