Ticker

6/recent/ticker-posts

SPIKA DKT. TULIA AWASILI GHANA KUSHIRIKI MKUTANO WA CPC

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 3 Oktoba, 2023 amewasili Accra nchini Ghana na kupokelewa na mwenyeji wake Spika wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Alban Bagbin.

Dkt. Tulia anatarajia kushiriki Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) utaofanyika nchini humo kuanzia tarehe 3-6 Oktoba, 2023 yenye dhima isemayo “Miaka 10 ya Mkataba wa Jumuiya ya Madola: Maadili na Kanuni za kuzingatiwa na Mabunge”

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na kuzungumza na Spika wa Bunge la Ghana Mhe. Alban Bagbin wakati alipowasili katika Jiji la Accra, Ghana ambapo anatarajia kushiriki Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) utaofanyika nchini humo kuanzia tarehe 3-6 Oktoba, 2023.

Post a Comment

0 Comments