NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kuelekea Maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Jinsia nchini TGNP Wadau wa Jinsia na Maendeleo GDSS wameendelea kujivunia jukwaa lao ambalo linawapatia fursa ya kupaza sauti inayoleta fursa kuwa na haki na usawa kwa jinsia zote.
Akizungumza leo Oct 17,2023 kakatika semina za jinsia na maendeleo GDSS Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi amesema mtandao wa jinsia ulipoanzishwa mwaka 1993 ilikuwa ikiratibu majukwaa mbali mbali ambayo yateleta sauti za pamoja na jukwaa la kwanza ambalo lilianzishwa ni semina za jinsia na Maendeleo yaani GDSS ambalo lipo hai.
"Leo tumekutana ili kutafakari katika hizi semina za jinsia na Maendeleo GDSS tumefanikiwa wapi?Changamoto ziko wapi?tufanye Nini? ili tuweze kwenda miaka 30 inayo kuja"Amesema
Aidha Bi. Lilian amesema kuwa jukwaa la GDSS limeleta mageuzi makubwa ambapo limechangia watu wengine kuanzisha taasisi zao ambazo zimechangia mabadiriko katika ngazi za jamii.
"Tutatengeneza chapisho ambalo litaonesha Ni jinsi gani hili jukwaa limeta mabadiriko makubwa ili hata vizazi vijavyo vione umuhimu wa kuwa na majukwaa ya sauti za pamoja"Amesema.
Kwa upande wake Mjumbe wa semina hiyo Hussein Wamaywa amesema Semina hizo zimeleta mabadiriko kwenye jamii vitendo vya ukatili vimepungua,hivyo elimu ni Jambo la msingi kwani itachangia watu kuwa na uelewa sawa.
"Mfano Mimi kwenye familia yangu sahivi nitofauti na zamani nilivyo kuwa,Sasa hivi na weza kukaa na familia yangu tukapanga bajeti masuala ya mapato na matumizi,hata kutenga bajeti tunaangalia,tunavyo mpangia bajeti ya mtoto wa kike sio sawa na ya mtoto kiume"Amesema
Pamoja na hayo amesema kuwa semina hizo zimeleta mabadiriko makubwa katika maeneo mbali mbali kupitia semina hizo zime changia katika suala la uzazi salama,katika mkoa wa Rukwa kulikua hakuna hospitali baada ya kuzungumza na wananchi waliweza kutoa nguvu zao katika ujenzi na serikali kuchangia mabati.
Semina hizo za jinsia na maendeleo zinafanyika kila Jumatano katika ofisi za Mtandao wa jinsia nchini.
0 Comments