Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI BYABATO AIPONGEZA BANK YA NMB,ATAKA USHIRIKIANO UENDELEE.



Na Shemsa Mussa, Kagera.

Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Stephen Byabato ametoa shukrani kwa uongozi wa bank ya NMB kutokana na kujitoa kwenye huduma mbali mbali za kijamii.

Amesema hayo katika hafla ya upokeaji masaada wa madawati ,viti ,meza ,mabati na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na bank hiyo katika uwanja wa shule ya sekondari Rwamishenye,pia amesema kwa upande wa Manispaa ya Bukoba wamepokea zaidi ya jumla ya madawati yenye thamani ya shilingi Milioni 26 na kuwaomba na kuwasisitiza watumiaji na wasimamizi wa vifaa hivyo kuvitunza vizuri kwani bado huitaji ni mkubwa .



Byabato ameongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia Wanafunzi kusoma bila vikwazo huku akiwaomba NMB kuendelea kuwashika mkono kwenye masuala mbalimbali ikiwemo elimu, Afya na ushirikiano wa kiuchumi na hata michezo.


"Niwaombe Mwendelee kutushika mkono maana mambo yapo mengi sana kwa upande wa elimu tunayo shule ya Msingi Byabato ipo Kashai, shule ya Sekondari Bukoba Bweni la Wanafunzi wa kike liko katikati ya mji na halina uzio tunaomba msituchoke tushirikiane kwa pamoja mfanye yetu na sisi tufanye yenu " amesema mbunge huyo wa Jimbo la Bukoba mjini.


Naye Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza amewashukuru NMB kwa kutimiza wajibu wao kwa umma pia kwa kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan na kueleza kuwa miaka mitatu iliyopita Nchi nzima ilikuwa na shida kwa baadhi ya Wanafunzi kukaa chini kutokana na ukosefu wa madawati na viti licha ya Serikali kulipambania vyema suala hilo huku akiiomba Benki hiyo kuzisaidia baadhi ya shule za Wilaya ya Bukoba ikiwemo Kyamulaile Sekondari na Kibirizi sekondari kuwawezesha upande wa ujenzi wa Bweni kwani wanafunzi utembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.


Aidha Meneja NMB kanda ya ziwa Dickson Richard amesema kuwepo kwa Benki hiyo ni sehemu mojawapo ya jamii hivyo watahakikisha wanaendelea kuirudishia jamii kitu cha mfano ambapo hadi sasa wameenda mpaka kupanda miti kwa ajili ya kutunza Mazingira ambapo wanatarajia kuendeleza mradi wao wa kupanda miti ili ndani ya mwaka 2023 wawe wamepanda miti Milioni 1ikiwa tayari mpaka sasa wameshapanda miti zaidi ya laki 5.


Akizungumza kwa niaba ya walimu waliopokea vifaa hivyo Mkuu wa shule ya Sekondari Rwamishenye yalipofanyika makabidhiano Aireth Philemoni Munisi ameishukuru bskk hiyo na amesema kwa upande wake amepokea viti 100 na madawati 100 kwa shule yake pia kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa madarasa mapya 8 huku akiitaja shule hiyo kukabiliwa na changamoto za uhaba wa matundu ya vyoo kwa Wanafunzi wa kike na wa kiume, kifaa cha kuandaa mitihani kwa Wanafunzi (photocopy Mashine) ambapo pia aliiomba Benki hiyo kuendelea kuwashika mkono ili kupunguza mapungufu madogo madogo.

Post a Comment

0 Comments