Mradi wa kuchukua data za mitetemo za 2D katika kitalucha Eyasi Wembere umefikia mwisho huku wataalamuwakielezakuwa na matumaini ya utafiti huo kubainisha na kuainishamaeneo yenye viashiria vya uwepo wa rasimaliya mafuta.
Hayo yamebainika hivi karibuni wakati wa ziara yaufuatiliajiiliyofanywa na Maafisa wa Mamlaka ya udhibitiMkondo waJuu wa Petroli (PURA) katika eneo la EyasiWembere mkoaniSingida ambapo mradi huo umekuwaukitekelezwa.
Akizungumza na maafisa hao Bw. Sindi Maduhu, Mjiofizikiawa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Meneja Mradihuo ameeleza kuwa utafiti huo wa 2D umefanyika katikamaeneo yaliyopo katika wilaya sitazilizo ndani ya mikoamitano ambayo ni Singida, Arusha, Tabora, Shinyanga na Simiyu.
“Tuna matumaini makubwa kuwa utafiti huuutatusaidiakubainisha na kuainisha maeneo yenyeviashiria vya uwepo wamafuta na gesi asilia na endapotutagundua viashiria na kujiridhisha na uwepo warasilimali hiyo, hapo ndipo itaanzahatua muhimu yakuchoronga visima vya utafiti zaidi,” alisema.
Akieleza historia fupi ya utafiti wa mafuta kwenye bondehilo la Eyasi Wembere Bw. Maduhu ameeleza kuwa utafitiulianzamwaka 2015 kwa kuchukua taarifa za kijiofizia(gravity magnetic) ili kubaini ukubwa wa eneo la bondena kuangaliakina cha miamba tabaka iliyopo katika eneohusika.
Eneo la Eyasi Wembere lina kilometa za mraba 10630, na utafitihuo ulilenga kusoma aina na kina cha miamba ilikubainiuwezekano wa uwepo wa mafuta au gesi asiliakatika eneohusika.
Utafiti katika bonde hilo umekuwa ukiendelea kufanyikakwavipindi tofauti tofauti na kwa kutumia teknolojiambalimbaliambapo kufikia mwezi Julai 2023 utafiti wadata za mitetemokwa njia ya 2D ulianza rasmi kwenyeeneo hilo.
Bw. Maduhu alifafanua kuwa utafiti wa data za mitetemo(2D) ni ule wa kutuma mawimbi ya sauti ardhini na mawimbi hayohurudisha taarifa ambazo baadayehuchakatwa na kutafsiriwa ilikuielewa miamba ya eneohusika na hivyo ili kujiridhisha na viashiria vya uwepo wamafuta.
Akizungumzia ushiriki wa wazawa kwenye mradi huo, Bw. Maduhu amesema Watanzania wengi wamenufaika na nafasi zaajira katika kipindi chote cha utekelezajimathalani mwaka 2022 zaidi ya Watanzania 40 waliajiriwa kwa ajira za muda ilikufanya kazi ya kukusanyataarifa za kijiokemia.
Aidha alibainisha kuwa tangu kuanza utafiti wa 2D mweziJulai, zaidi ya Watanzania 250 wamepata ajira katikamradi huo hukutakriban asilimia 98 ya kazi za kitaalamuzikifanywa na wazawaikiwa ni pamoja na kazi zakuendesha mitambo hukuikilinganishwa na asilimia 2 pekee iliyohusisha raia wa kigeni.
“Kwa upande wa manunuzi zaidi ya asilimia 60 yakandarasizilizotumika katika utekelezaji wa mradi huo niza kampuni zaKitanzania ikiwa ni pamoja na kampuni yaAfrica Geophysical Services (AGS) ambayo ndiyemkandarasi aliyefanya utafitihusika wa 2D kwenye mradihuu,” alieleza.
Aliongeza kuwa kandarasi ndogondogo za kutoa hudumakamachakula, ulinzi na nyinginezo ndizo zilizopewakipaumbelekwenye mradi huo ikilinganishwa na kampuniza kigeni.
Mradi huu wa kuchukua data za mitetemo katika bondehilo la Eyasi Wembere umegharimu kiasi cha Shilingi zaKitanzaniaBilioni 8 ambazo zimetolewa na Serikali kupitiaTPDC
0 Comments