Katika kuhakikisha jamii inafahamu maswala ya uzazi wa mpango hasa kundi muhimu la vijana Marie Stop Tanzania imekita Kambi Katika Maonesho ya wiki ya vijana yalionza Oktoba 8, 2023 Mpka Oktoba 14, 2023 Ili kuwafamisha njia zilizo sahihi.
Katika kuhakikisha vijana wanajitambua na kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango Marie Stop Tanzania inatumia mbinu mbalimbali ambazo zinavutia vijana kujifunza na kufahamu kuhusu uzazi wa mpango na Afya ya uzazi kwa ujumla.
Akizungumza na vijana katika banda lao Afisa Usawa wa Kijinsia,Vijana na Ujumuishaji Jamii Ndugu Denice Simeo amesema " Tukiwa kama wadau wa Maendeleo ya Vijana, maadhimisho haya ni fursa muhimu kwetu kukutana na vijana kuwaeleza kuhusu swala la Afya ya uzazi na watambue njia sahihi za kujilinda na Majongwa, Mimba zisizotarajiwa na Mimba za utotoni"
Licha ya hayo wanaendelea kutoa elimu na mafunzo yatakayofanya vijana kujilinda na kuelewa kwa undani kuhusu Afya ya uzazi
Pia wanawafundusha wadau mbalimbali wanaotembelea Banda lao katika Maonesho hayo kuhusu faida lukuki kuhusu namna Bora za kujilinda ikiwa ni pamoja na kuja bidhaa ya Life Guard Condom Ili kuhakikisha vijana wanakuwa salama
0 Comments