Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS AKIKABIDHI HATI ZA KIMILA WILAYANI MAKETE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhi hati za kimila kwa wawakilishi wa wakulima wa ngano waliopimiwa ardhi kwenye mpango wa kilimo cha ngano Wilaya ya Makete wakati akiwa ziarani mkoani Njombe leo tarehe 27 Oktoba 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wakulima wa ngano waliopimiwa ardhi kwenye mpango wa kilimo cha ngano Wilaya ya Makete mara baada ya kukabidhiwa hati za kimila. (wa kwanza kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi kutoka kwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati – Makete Dkt. Wilson Sanga iliyotolewa na watu wenye mahitaji maalum mara baada ya kuzindua mradi wa kufua nishati ya umeme wa KV 360 unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliopo Kijiji cha Masisiwe wilayani Makete mkoani Njombe. (tarehe 27 Oktoba 2023).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa katika picha ya pamoja na Bi.Ronesta Mgaya mkazi wa Tandala Wilayani Makete mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Wilaya hiyo akiwa ziarani mkoani Njombe leo tarehe 27 Oktoba 2023.

Post a Comment

0 Comments