Ticker

6/recent/ticker-posts

WCF YAENDESHA MAFUNZO YA UELEWA WA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA ZIWA NA WAKURUGENZI WA CMA

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MWANZA

MAJAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Ziwa na Wakurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) wameanza kikao kazi kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili kuwajengea uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Kifungu cha 5 [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015].

Kikao hicho kilichofunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, Septemba 15, 2023, jijini Mwanza, kinafuatiwa na kikao kama hicho kilichofanyika Juni 9, 2023 mjini Bagamoyo na kuhudhuriwa na Majaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, kutoka Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, pamoja na wakurugenzi wa CMA.

Akizungumza na washiriki hao, Dkt. Mduma amesema, Mahakama ni chombo muhimu katika mchakato wa ulipaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi walizoajiriwa kwa mujibu wa mkataba

Amesema, mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuzitaka taasisi za umma kuongeza ufanisi na ubora wa utoaji huduma kwa wananchi.

“Kwa hivyo Mahakama na CMA ni wadau muhimu katika utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi lakini pia tunajenga uelewa wa pamoja, kikao kazi hiki, kitaleta manufaa makubwa ikiwemo kuimarisha mahusiano, kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi na kuchangia kwenye kukuza uchumi wa nchi yetu.” Alifafanua Dkt. Mduma.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina ameipongeza Menejimenti ya WCF kwa kuwa tayari kushirikiana na Mahakama pamoja na taasisi zinazohusu utatuzi wa migogoro ya kazi katika eneo la kujenha uelewa wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Alisema, mafunzo hayo yatasaidia sana taasisi hizo kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya sheria zinazohusu ulipaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia au kuugua wakiwa kazini au kwa familia za wafanyakazi wanaofariki kutokana na ajali wakiwa kwenye ameneo yao ya kazi.

“Mheshimiwa Jaji Mkuu alifanya ugatuzi kwa kuelekeza Waheshimiwa Majaji wote wa Mahakama Kuu ya Tanzania Manaibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wote, kwa sehemu ambazo hazina Masjala ya za Mahakama Kuu kushughulikia mashauri ya Kazi, hivyo niliwaomba WCF watuandalie mafunzo mengine ya kikanda na nashukuru leo tuko hapa Mwanza.”

Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA, Bw. Thomas Malekela, alisema tume inashughulikia haki zilizovunjwa mahali pa kazi.

“Mfanyakazi anaweza akalalamika juu ya mshahara ambao kwaweli si wenyewe, anazungumzia mshahara pamoja na mamslahi, CMA ikitoa uamuzi kuwa mshahara wako halisi ni huu na ndio utakaozingatiwa, WCF itatumia uamuzi huo wa CMA katika kutekeleza jukumu lake la kulipa fidia.” Alifafanua Bw. Malekela.

Pamoja na kujifunza sheria ya fidia kwa wafanyakazi, maeneo mengine ambayo Majaji hao pamoja na wakurugenzi wa CMA wamejifunza ni taratibu za Madai ambapo wamepata fursa ya kuelezwa jinsi tathmini za madhara ambayo mfanyakazi ameyapata zinavyofanyika.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (kulia) akipeana mikono na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina baada ya kufungua kikao hicho
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, akizungumza na washiriki.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Ziwa, wakisikiliza maelezo ya ufunguzi wa kikao hicho

Mkuu wa Huduma za Sheria, WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi nchini, (WCF).
Washiriki wakiwa katika kikao hicho.

Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akijibu baadhi ya hoja kuhusiana na Tathmini za Madai.
Meneja Madai WCF, Bi. Rehema Kabongo, akitoa mada kuhusu taratibu za Madai

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (katikati) na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe Dkt. Ntemi Kalekamajenga.

Baadhi ya washiriki

Baadhi ya washiriki

Afisa Mwandamizi wa Huudma za Sheria, WCF, Bw. Deogratius Ngowi

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kulia), Mkuu wa Huduma za Sheria, Bw. Abraham Siyovelwa (wapili kulia) na watumishi wengine wa WCF, wakimsikilzia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Bi. Laura Kunenge

Mkurugenzi Mkuu, WCF Dkt. John Mduma (katikati waliokaa), akiwa na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, wakiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina (wapili kushoto waliokaa). Wakwanza kulia waliokaa ni Kaimu Mkurugenzi wa CMA, Bw. Thomas Malekela

Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mahakama na Wakurugenzi wa CMA.

Meza Kuu wakiwa na watendaji wa WCF.

Post a Comment

0 Comments