Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAHABARI ZAIDI YA 200 KUTOKA NCHI 14 KUSHIRIKI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SABA ZANZIBAR

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAKUU wa Vyombo vya Habari vya Umma, Wadau wa TEHAMA na Wanahabari zaidi ya 200 kutoka nchi 14 wanachama Kusini mwa Afrika , Afrika Mashariki na Magharibi wanatarajia kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.

Mkutano huo wa 30 wa mwaka wa SABA na Mkutano wa 7 unazungumzia masuala ya TEHAMA katika kukuza teknolojia ya Habari na Utangazaji Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba amesema mkutano huo utajadili kwa kina nafasi ya TEHAMA na mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa kidijiti Afrika ili kuleta maendeleo endelevu na kuonyesha maboresho makubwa yaliyofanyika hivi karibuni katika teknolojia ya Habari.

"Lengo lingine ni kujadiliana habari, kupanua uelewa wa masuala ya TEHAMA na kupeana mbinu mbalimbali za kuboresha teknolojia ya habari na utangazaji ili kuendana na mabadiliko kiteknolojia ya sasa". Amesema

Aidha amesema kuwa Mkutano huo utafanyika katika hoteli ya Golden Tulip ambapo mgeni rasmi ambaye atafungua anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Umoja na Mashariki ya Utangzaji ya Umma Kusini mwa Afrika (SABA).

Pamoja na hayo amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania kwa kuwa utachangia ongezeko la pato la Taifa linalotokana na Utalii.

"Tumeichagua Zanzibar kwa kuwa ni mojawapo ya maeneo muhimu ya utalii katika nchi yetu. Wageni hawa watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Zanzibar na kujionea uzuri na upekee wa eneo hili la nchi yetu". Amesema

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments