Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services (TFS),wamewaalika watanzania wote kutembelea misitu ya TFS maana kuna vivutio vizuri na mazingira yake ni yakuvutia.
Akizungumza katika kilele cha hitimisho ya wiki ya Kongamano la pili la kitaifa la ufuatiliaji, Tathimini na mafunzo Bi.Anna Lawuo ambaye pia ni Afisa mtalii amesema kuwa TFS wanavyovivutio vingine mbali na tofauti vile ambavyo wamevizoea ambavyo n vivutio vya utalii Ikolojia vinavyopatikana ndani Misitu ya hifadhi hiyo ikiwemo ziwa lenye ramaniya Afrika.
Vilevile Bi.Anna amesema kuwa ndani ya misitu hiyo kuna fursa za uwekezaji na upatikanaji wa bidha za nyuki ambapo kutokana na mizinga hiyo ya nyuki inaweza kuwapatia faida kwasababu mizinga hiyo inatoa bidhaa mbali mbali zinazotokana na nyuki ikiwemo asali na nta ambayo wameitumia kutengenezea bidhaa mbalimbali zinazotokanazo na nta hiyo ya nyuki.
Pamoja na hayo alisema kuwa kwa wale watanzania wanaofanya mazoezi barabarani wanauwezo wakwenda kufanyia mazoezi katika misitu hiyo kwasababu hali ya hewa iliyopo maeneo hayo ni nzuri na nisafi pia kwa afya ya mtu yoyote "Tunawaomba wale wanaofanya mazoezi mijini wanaofanya kwenye barabara sehemu ambazo kunamwingiliano wa watu wengi na magari si salama sana kwa afya lakini wakija maeneo ya msituni watakutana na hewa safi na utakuwa umepumzika kwa kuvuta hewa safi ambayo haitaathiri mwili wako"alisema.
Hata hivyo alimazia kwakusema kuwa watalii na watanzania wote wanakaribishwa katika misitu hiyo kwasababu kuna maeneo ya kempu na mandhari yakuvutia huku kiingilio chake kikiwa rahisi kwa mgeni na mtanzania yoyote atakaetamani kutembelea vivutio hivyo.
Naye mhifadhi mwandamizi kutoka TFS,Kelvin Fella amesema kuwa ndani ya utalii ekolojia kuna hifadhi za malikale kuna vivutio vingi vyakuanzia enzi za ukoloni mpaka tulipopata Uhuru kukiwa na vituo tofauti kama mji mkongwe unaopatikana Bagamoyo ikiwa ndo mji mkuu wa kwanza vikiambatana na magofu ya kaole aambayo ni vivutio vikubwa kwa watali.
Alisema kuwa kutembelea vivutio hivyo ni garama nafuu "katika hifadhi za Bagamoyo na Kaole ni kiingilio nafuu kwa Mtanzania ni Shilingi elfu mbili tu huku mgeni ni elfu ishirini ya Kitanzania na kwa mgeni ambaye ni wa moja kwa moja atalipa elfu kumi tu unaweza kulipa na kupata historia katika vivutio hivyo "alisema.
0 Comments